MEYA
wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kinyang’anyiro
cha kumsaka Redd’s Miss Ilala 2012 kitakafanyika leo kwenye ukumbi wa
Nyumbani Lounge Namanga jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Redd’s Miss Ilala 2012, Juma Mabakila,
alisemba Miss Ilala mwaka huu, atazawadiwa sh
milioni 1.5, mshindi wa pili sh mil 1.2 wa tatu sh 700,000 wa
nne
na wa tano watapatia sh 400,000 kila mmoja huku waliobakia watapata kifuta
jasho cha sh 200,000.
Aidha kutakuwa na burudani kutoka kwa msabnii nguli wa kizazi kimpya nchini Lady Jaydee na
Machozi Band, Banana, Ommy Dimpoz na Chege.
Warembo
watakaopanda jukwaani leo kumrithi Salha Israel
ambaye pia ni Miss Tanzania ,
ni Mary Chizi, Matilda Martin, Mgdalena Munisi na Suzan Deodatus.
Aliwataja warembo watakaowania taji hilo ni pamoja na Whitness Michael, Stella Moris, Elizabeth Perty, Wilmina Mvungi, Zawadi
Mwambe, Rehema Saidi, Diana Simon,Amina Sangwe, Noela Michael na Phillios Lemi.
Shindano hilo limedhaminiwa na City Sports Lounge, Redd's Premium Cold, Uhuru One,
Dodoma Wine, Nyumbani Lounge, 100.5 Times FM, 88.4 Cloud's FM, Uhuru One,
Dodoma Wine, Nyumbani Lounge na Amaya Salon.