Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya
Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanne waliokuwa wakichezea timu
mbalimbali nchini.
Wachezaji hao ni Tony Ndolo aliyejiunga na KCC ya Uganda
kutoka Toto Africans, Felix Amech Stanley aliyekwenda Bahla ya Oman kutoka
Coastal Union, Ernest Boakye kutoka Yanga aliyejiunga na Tripoli Athletics Club
ya Lebanon na Derrick Walulya aliyerejea URA ya Uganda kutoka Simba.