Twite
SAKATA
la Simba kurejeshewa dola 32,000 za usajili wa beki wa kimataifa wa Yanga,
Mbuyu Twite limechukua sura mpya baada ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF)
kulirudisha tena kwa kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF.
Hatua
hiyo inafuatia kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa kuipa Yanga
siku 21 kuirejeshea Simba fedha hizo, lakini mpaka kipindi hicho kinamalizika
wiki iliyopita Yanga ilishindwa kutimiza maelekezo hayo.
Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema kwamba
baada ya kuona kimya kuhusiana na deni lao waliandika barua TFF ili kuomba
msaada wa jambo hilo.
Alisema
TFF iliwataka kusubiri mpaka kamati ya kina Mgongolwa itakapoketi kwani ilibidi
suala hilo walirejeshe tena katika kamati hiyo kutokana na awali kutotoa
mwongozo nini kifanyike iwapo Yanga ingeshindwa kulipa deni katika siku
ilizopewa.
Kamwaga
aliongeza kwamba wanasikitishwa na kitendo wanachokifanya Yanga kwani suala
hilo halikupaswa kufikia hatua iliyopo sasa.
Naye
Katibu Mkuu wa Yanga Lawrance Mwalusako alipozungumza na mwandishi wa habari
hizi kuhusiana na suala hilo, alidai hawezi nkulizungumzia kwani lipo ndani ya
uongozi wa klabu hiyo.
Awali,
Simba ilimsajili Twite kutoka klabu ya APR ya Rwanda ambayo alikuwa akiichezea
kwa mkopo kutoa FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kwa dau la
dola 32,000 kabla ya Yanga kumpandishia dau la dola 50,000 na hivyo kumwaga
wino.
Hata
hivyo, Simba ilikuja juu kwa madai Yanga ilivuruga usajili huo, huku Yanga nayo
ikitumia maarifa zaidi ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Lupopo ambayo ndiyo
yenye mamlaka na Twite na si APR kama ilivyofanya Simba.
Kama
hiyo haitoshi, baadhi ya viongozi wa FC Lupopo walikuja jijini Dar es Salaam
ili kuwarejeshea Simba fedha zao lakini viongozi wa Simba waligoma na kudai
hawakutoa fedha hizo kwa uongozi wa Lupopo hivyo wanataka Twite mwenyewe
arudishe fedha hizo.