msemaji wa Simba,Ezekiel Kamwaga
KLABU ya soka ya Simba ipo mbioni kuvichukulia hatua za kisheria baadhi ya vyombo vya
habari ikiwemo mitandao ya kijamii ambayo inaendesha zoezi la kumchafua kiungo wao, Haruna Moshi ‘Boban’
baada ya kumkwatua nyota wa Yanga, Kelvin Yondan katika mchezo baina ya timu
hiyo jumatano iliyopita.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba anashangazwa na mchakato huo kwani kitendo alichokifanya
Boban ni sehemu ya mchezo na ndiyo maana mwamuzi alitoa adhabu iliyostahili.
"Hata wachezaji wenyewe walishalizungumza hilo na na kusameheana lakini baadhi ya mitandao
imekuwa ikimuandika Boban kama amefanya tendo
la unyama.
Kamwaga alisema wanawasiliana
na mwanasheria wao ili kulifanyia kazi suala hilo
ambalo kama likifumbiwa macho linaweza kuleta
athari kubwa kwa jamii.
Katika mchezo huo wa ligi kuu bara uliopigwa uwanja wa Taifa jijini dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, huku Yondan akilazimika kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili kutokana na kuumizwa na Boban.