Kocha mkuu wa Mabingwa wa klabu Bingwa Afrika Mashariki na
Kati, timu ya Young Africans Sports Club Mholanzi Ernie Brandts amesema kikosi
chake kipo tayari kuikabili timu ya Simba sc katika mchezo wa ligi kuu ya
Vodacom hapo kesho uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam .
Akiongea na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz. leo
asubuhi katika mazoezi ya mwisho yaliyofanyika shule ya sekondari Loyola,
amesema wachezaji wake wote wapo safi ,
wana ari ya mchezo na ushindi, hivyo anaamini mchezaji yoyote atakayempanga
atafanya vizuri.
Yanga mabingwa watetezi wa kombe la Kagame mara mbili
mfululizo, wataingia uwanjani kusaka point 3 muhimu ambazo zitaipelekea kusogea
katika nafasi nzuri ya kutwaa Ubingwa msimu wa 2012/2013.
Katika mazoezi yaliyofanyika leo asubuhi, kocha Brandts
aliweza kuwatumia wachezaji wote waliosajiliwa katika msimu huu wa ligi,
isipokuwa Salum Telela pekee ndio mchezaji majeruhi .
Kocha Brandts amesema amefurahi kwa wachezaji wake wote kuwa
fit, kiakili, kimwili na kifikra kwa ajili ya mchezo wa kesho, na hivyo
anawaahid wapenzi na wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kuona soka safi na
la kuvutia.
Mchezo utaanza majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika
Mashariki na utaonyeshwa moja kwa moja dunia nzima na kituo cha runinga cha Supersport cha
nchini Afrika Kusini.
'MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU IBARIKI YOUNG
AFRICANS'
'DAIMA MBELE NYUMA MWIKO'
CHANZO:www.youngafricans.co.tz