KLABU
ya Yanga imeeleza kusikitishwa kwa kutangzwa kwa mapato kiduchu katika mechi
yao dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba na kulitaka Shirikisho la soka
Tanzania (TFF) kulifanyia uchunguzi wa kina suala hilo.
Hatua
hiyo inafuatia TFF kutangaza mapato ya sh. milioni 390, 568,000 ambayo yalitokana na watazamaji 50,455 waolikata tiketi
kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000,
sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Katibu Mkuu
wa Yanga Lawrance Mwalusako alisema kwamba hali hiyo inatia shaka kwani hata
takwimu za idadi ya watazamaji zilizotolewa na TFF ni tofauti na ile ya kituo
cha Televisheni cha Supersport ambacho kilionyesha kuwa lilihudhuriwa
na mashabiki 59000.
Alisema
kwa hesabu za haraka haraka hata mashabiki waliohudhuria mechi hiyo wangelipa
15,000 kila mmoja zingepatikana zaidi ya shilingi milioni 600 hivyo hata vilabu
husika vilistahili kupata zaidi ya milioni 93,345,549.15 walizogawiwa kila klabu kama sehemu ya mapato
hayo.
Mwalusako
aliongeza kwamba wanashindwa kuelewa hali hiyo inatokana na nini na kuiomba TFF
kufanya uchunguzi wa haraka ili kujua tatizo linatoka wapi, lakini kinyume na
hapo hali itazidi kuwa mbaya.
Katibu
huyo aliongeza kuwa wanatarajiwa kuwasiliana na viongozi wenzao wa Simba ili
kujadili hali hiyo kabla ya kutoa tamko la pamoja.