WAKATI uongozi wa klabu ya Simba ukisikitishwa na mwenendo mbaya wa timu hiyo katika mzunguko wa ligi, umejipanga kusajili wachezaji wataokaoingezea makali timu hiyo, huku pia
wakitaraji kuopunguza wachezaji kadhaa.
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema leo kwamba,katika harakati za
usajili wa usajili wa dirisha dogo wanampango wa kumrejesha beki wake wa zamani
wa kimtaifa Mkenya, George Owino kutoka Azam Fc na kumpeleka huko kiungo wao,
Uhuru Suleiman.
“Tupo katika mazungumzo na
uongozi wa Azam Fc ambayo yapo katika hatua nzuri na muda si mrefu tutasaini
mkataba rasmi kuhusiana na hatua hiyo,”alisema