Kampuni ya Precision Air kwa kushirikiana na kampuni
ya bia ya Serengeti, na SBC (Pepsi) T Limited wamedhamini mashindano
ya gofu ya Johnnie Walker Waitara yatakayo fanyika mwisho wa wiki hii.
Mashindano
haya maarufu kama Johnnie Walker Waitara Trophy yatafanyika kuanzia
ijumaa na jumamosi wiki hii katika viwanja vya gofu vya Lugalo.
Mashindano
hayo yatashirikisha wachezaji 120 watakaoshindania kikombe na fedha
taslimu huku washindi wengine watano wakijishindia tiketi tano za ndege
kutoka Presicion Air.
Akizungumza wakati wa kuzindua michuano hiyo, Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Emilian Rwejuna, amesema kampuni hiyo imekuwa mdhamini mkubwa wa mashindano hayo kila mwaka.
“Tunathamini
mchezo wa gofu nchini na wachezaji kwa ujumla na ndio maana tumeamua
kujikita katika mchezo huu. Mbali na kudhamini mchezo wa gofu. Johnnie Walker imekuwa
ikijihusisha na michezo mingine kama mashindano maarufu ya langalanga
kupitia timu ya Mclaren Mercedes yenye wachezaji kama Lewis Hamilton
na Jenson Button, na pia Johnnie Walker imekuwa ikijihusisha na watu
maarufu katika michezo na sanaa zingine kama wanariadha maarufu
Gabriel Haile selasie,
Manu Dibango na wengine wengi. Johnner Walker ina kauli mbiu yake ya KEEP WALKING.
Mratibu wa masoko wa kampuni ya Precision Air, Hillary Mremi amesema kuwa kampuni yao iko katika msitari wa mbele kukuza vipaji na michezo nchini.
“Tumejipanga
vyema kuhakikisha tunachangia maendeleo ya michezo nchini, kwani
wanamichezo wetu ndio mabalozi wazuri kwa nchi yetu hivyo ni jukumu letu
kuwasaidia wao kufanya vizuri,” alisema Mremi.
Tunajisikia fahari kuwa sehemu ya mashindano haya, kwani itakuwa ndiyo njia pekee ya kukuza mchezo nchini.”
Wengine
waliokuwa katika uzinduzi ho ni pamoja na Foti Gwebe Nyirende, Mkuu wa
huduma za jamii wa SBC, watengenezaji wa kinywaji cha pepsi ambao pia ni
wadhamini wa mashindano hayo.