MWENYEKITI wa klabu ya Simba
Alhaj Ismail Aden
Rage amesema kwamba uongozi umebaini kwamba wengi wa wanachama wa tawi la Mpira
Pesa waliojiorodhesha ili kushinikiza kufanyika kwa mkutano wa dharura wa klabuu hiyo si hao.
Hatua hiyo inafuatia
wanachama hao kufanya maadhimio ya kujiorodhesha ili kufikisha akidi
itakayotimiza mashaerti ya kufanyika kwa mkutano ili kuwaonmdoa madarakani
viongozi wa sasa kwa madai ya kushindwa kuongoza.
Rage amesema pamoja na kubaini hilo , pia uongozi
umegundua kwamba majina ya wanachama hao
yamenakiliwa katika leja ya wanachama ambayo ilipotea mikononi mwa kiongozi
mmoja wa zamani.
Alisema uongozi unaheshimu
jitihada zinazofanywa na wanachama hao na kuzifanyia kazi, lakini hauwezi
kutekeleza vitu ambavyo havikidhi vigezo vilivyopo katika katiba ya klabu hiyo.
Rage alisema, katiba ya sasa
ya Simba haiwatambui wanachama waliopo kwenye leja, badala yake inawatambua
wale waliosajiliwa katika kompyuta.
“Pamoja na wanachama hao
kunakiliwa katika leja,tumebaini hata saini zilizowekwa ni za kughushi na
tukifanya uchunguzi hasa tutabaini ni wengi tu hawana sifa, kitu ambacho kinakwenda kinyume na katiba ya
Simba,”alisema Rage
Rage aliongeza kuwa,
wanaamini mchakato huo unafanywa na baadhi ya watu wanaotaka kuleta chokochoko
ndani ya klabu hiyo kitu ambacho ni kigumu kukitimiza kwa vile uongozi upo
imara na unafuata katiba ya klabu hiyo.
“Hatuwezi kujiuzuilu kwa
ajili ya shinikizo la watu ambao tunafahamu wanatumika, sisi tunaongoza kwa
kufuata katiba na tutachukua uamuzi kwa mujibu wa katiba pindi inapostahili,”alisema
Aidha, Rage aliongeza kwamba
uongozi wa klabu hiyo ulitarajiwa kukutana jioni ya jana kwa ajili ya kujadili
masuala mbalimbali ikiwemo mwenendo mbaya wa timu hiyo katika mzunguko wa
kwanza wa ligi kuu ya Vodacom uliomalizika wiki iliyopita na Simba kushika
nafasi ya tatu.
Hivi karibuni baadhi ya
wanachama waliutakla uongozsi wa Simba chini ya Rage kuachia ngazi baada ya
timu hiyo ambayo ilikuwa ikiongoza ligi kwa kipindi kirefu kupoteza mwelekeo
baada ya kupoteza michezo yake.