Fainali
ya tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka
zinazotolewa na Kampuni ya Wazalendo Bright Media zinatarajiwa kufanyika
Desemba 30 mwaka huu jijini Dar es
Salaam katika sehemu (venue) itatangazwa baadaye.
Mchakato
wake ulianza tangu Agosti mosi mwaka huu kwa wanamichezo kupigiwa kura na
mashabiki kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo ile ya kijamii (face book,
Twitter na Blogs) na wengine kwa njia ya simu za mikononi kwa kupitia namba
maalum.
Kwa
sasa kamati ipo kwenye mchakato ya kuchuja majina ambayo yamependekezwa na mashabiki wa soka kupitia kura zao ambapo
zaidi ya wachezaji 93 wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara majina yao yameweza kuonekana
ambapo kati ya majina hayo yataopunguzwa na kufikia 30.
Aidha
kabla ya kufanyika kwa fainali hiyo wale wachezaji ambao wataingia kwenye
fainali watapatiwa semina ya uwezekezaji na ujasiriamali ili kujiandaa na
maisha ya baadaye baada ya kustaafu.
Sababu
za kufanya semina hii ni kuhakikisha kuwa wachezaji wetu wanapata elimu ya
uwezekaji na ujasiriamali ili kuwekeza kwenye sekta mbalimbali kwa ajili ya
siku zijazo hasa ikizingatiwa kwamba wachezaji wengi wa Tanzania bado ni masikini.
Kwenye
semina hiyo watakuwepo wataalam waliobobea kwenye mambo ya uchumi na fedha
ambao watatoa elimu ya uwekezaji, kwa kufanya hivi itawapa nafasi wachezaji
hawa kuelewa na kutambua umuhimu wa uwekezaji.
Semina
hiyo inatarajiwa kufanyika Desemba 19 na
20 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.
Pamoja semina ambayo itakwenda sambamba na
utoaji wa elimu ya afya kwa washiriki wa semina hiyo ambao watakuwa
wachezaji pekee.
Tuzo
za aina hii ni za kwanza kufanyika nchini Tanzania ambapo mshindi wa tunzo
hiyo anatarajiwa kuopata tuzo, fedha taslim, medali na cheti.
Imetolewa na
Ahadi Kakore- Mratibu
Novemba 20
2012