Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha
wachezaji 24 kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12 mwaka huu kuajianda kwa
mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika ,
Zambia .
Katika kikosi hicho, wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza
ni kipa Aishi Manula anachezea kikosi cha U20 cha Azam na timu ya Taifa kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), beki wa kushoto wa
Azam, Samih Nuhu, beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid na mshambuliaji
wa Azam, Mcha Khamis.
Pia kati ya wachezaji walioitwa, sita walikuwa kwenye kikosi
cha Zanzibar (Zanzibar Heroes) kilichokamata
nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Jumamosi
jijini Kamapala , Uganda . Wachezaji hao ni Mwadini
Ally, Nassoro Masoud Cholo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Samih Nuhu, Aggrey Morris
na Mcha Khamis.
Kikosi kamili kilichoitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba),
Mwadini Ally na Aishi Manula (Azam U20). Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba),
Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Samih
Nuhu (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Amir Maftah (Simba), Issa Rashid
(Mtibwa Sugar) na Kevin Yondani (Simba).
Viungo ni Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd Chuji (Yanga),
Mrisho Ngasa (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Mcha Khamis (Azam), Salum
Abubakar (Azam), Amri Kiemba (Simba) na Mbwana Samata (TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo- DRC).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga),
Thomas Ulimwengu (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Mwinyi
Kazimoto (Simba).
إرسال تعليق