NDOTO za Tanzania kushiriki fainali za Kombe la
Dunia 2014 nchini Brazil mwaka 2014 zilihitimishwa jana baada ya timu ya Taifa kutandikwa mabao 4-2 dhidi ya Ivory Coast katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
.Katika mchezo huo ambao Stars waliuanza vizuri, Amri Kiemba aliiandikia Stars bao la kwanza katika dakia ya kwanza ya mchezo huo
baada ya kupokea kazi nzuri ya Mbwana Samatta.
Dakika ya 12 Traore Lacina aliisawazishia Ivory Coast akimalizia krosi ya Yaya Toure, kabla ya Yaya kupachika la pili katika dakika ya 23
na dakika ya 34 Thomas Ulimwengu alisawazisha.
Kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi ya kupokezana huku Stars ikishindwa kuzitumia vema nafasi ilizozipata ndani ya kipindi hiyo na hatimaye dakika ya 90 Wilfred Bonny alihitimisha karamu la mabao kwa Ivory Coast kwa kupachikia la nne.
