Bodi ya taifa ya Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO), yenye dhima ya kikomo ya kuratibu na kuendesha Mashindano ya Miss Utalii Tanzania, imetangaza Kusimamisha kufanyika mashindano hayo katika
ngazi zote kwa msimu wa 2013/2014.
Lengo la kutofanya mashindano hayo
kwa mwaka mmoja ni kujipanga upya na kuboresha mfumo wa uendeshaji na
usimamizi wa mashindano katika ngazi zote.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo Erasto Gideon Chipungahelo, uamuzi huo mgumu umechukuliwa na bodi ya mashindano hayo wakati wa kikao cha tathimini
ya miaka mitano ya mashindano hayo, na miaka kumi ya taasisi ya Miss Tourism Tanzania Organisation ambayo ilisajiliwa na kuanzishwa rasmi mwaka 2002,sambamba na usajili wa mashindano hayo. Fainali za kwanza za Miss Utalii Tanzania, zilifanyika mwaka 2004katika ukumbi wa
Diamond Jubilee Dar es Salaam, na fainali za tano za Miss Utalii Tanzania zilifanyika Mei 19,2013 katika uwanja wa mkwakwani Tanga.
Bodi katika tathimini hiyo ya ndani imebaini changamoto mbalimbali za kimfumo,udhamini, utendaji,kuporomoka au kudumaa kwa sanaa ya urembo nchini na hujuma. Mfumo DUME wa uendeshaji wa mashindano ya urembo nchini kikwazo kwa ukuaji wa wazo au ubunifu wa kazi ya sanaa husika,kwani bodi imebaini mfumo huo kutoa mianya ya hujuma na kupindishwa kwa wazo na lengo mama la mbunifu.
Lakini pia mfumo DUME wa udhamini, umekuwa ni kikwazo na changamoto kubwa kwa ukuaji wa sanaa nchini, kwani mfumo uliopo wa udhamini unatoa fulsa ya wadhamini kuwa wafalme au miungu watu , kiasi cha kudhamini kisicho bora,kisicho na mafanikio, kisicho na tija katika jamii na kuacha kudhamini kilicho bora,chenye tija katika jamii na
kilicho na mafanikio makubwa kitaifa na kimataifa.
Kwa visingizio na sababu mbalimbali mfumo wa udhamini nchini umekuwa ukitoa fulsa kwA wadhamini kuwa waandaaji na kupotosha kabisa maudhui ya ubunifu wa sanaa husika. Mfumo wa udhamini nchini umezaa aina mpya ya Utumwa wa
kujitumikisha na kuwafanya wabunifu wa kazi za sanaa kuwa watwana na wadhamini kuwa mabwana mkubwa.
Kwa zaidi ya miaka 18 sasa tangu kuanza upya kwa sanaa ya urembo nchi,tumeshudia kuanzishwa na kufa au kuuawa kwa mashindano na kazi mbalimbali za ubuni fu wa sanaa hii. Aidha katika kipindi hiki tumeshudia kuporomoka kwa kasi ya ajabu kwa sanaa ya urembo nchini,tofauti na nchi jirani na nyinginezo duniani.
Kuporomoka ambako kumepelekea umaarufu wa matamasha ya urembo nchini kuporomoka.
Zipo sababu nyingi za kuporomoka kwa sanaa hii nchini, chache kati ya hizo ni Mfumo DUME wa Udhamini, kutotambua unyeti wa taaluma ya sanaa ya urembo kuwa ni wazo na ubunifu wa mtu kwa msukumo nafsi wa mtizamo,fikra na imani ya kuamini katika ndoto yake.
Hii inamaana kuwa tofauti na michezo au sanaa nyingine sanaa ya urembo hususani mashindano ya urembo hayana fomila wala mfumo yakini, kama ilivyo kwa mpira wa miguu,au muziki au uigizaji wa filamu, uchezaji na upigaji wa
ngoma za asili n.k, hivyo kwa kiasi kikubwa hutegemea ubunifu na mtizamo wa mbunifu wa shindano husika katika kufikia ndoto ya ubunifu na matarajio yakea juu ya wazo husika.
Bodi imebaini kuwa mifumo ya uendeshaji iliyopo inatoa mianya ya hujuma baina ya shindano na shindano na hata baina ya wadhamini wa shindano flani na jingingine, lakini pia baina ya wabubunifu na mafisadi wa kazi za sanaa za wabunifu wajasilia mali.
Hapa hujuma zimegawanyika katika makundi tofautitofauti ikiwemo waraembo mamluki wanao pandikizwa katika mashindano mengine, viongozi au wajumbe wa kamati mamluki na wale wenye uchu wa madaraka na kuvuna bila ya
kupanda, lakini hujuma kupitia propaganda chafu, Fitina,majungu na kupakana matope.
Zipo hujuma pia za watu wa kada mbalimbali katika jamii kutumiwa kufanikisha adhma ya mafisadi wa kazi za ubunifu wa sanaa na upindishaji wa sheria na taratibu za uendeshaji wa mashindano ya urembo duniani na sanaa nzima ya urembo kitaifa na kimataifa.
Udhamini na hujuma imekuwa ni changamoto kubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania.
Tofauti na mtizamo wa wengi kuwa tumekuwa tukipata udhamini na wadhamini wakubwa katika Miss Utalii Tanzania , ukweli ni kwamba hakuna udhamini wowote mkuu na
mkubwa tunao upata kutoka kwa sekta binafsi wala ya umma, badala yake tumekuwa tukitumia rasilimali zetu na nguvu zetu kufanikisha kufanyika kwa fainali za kila mwaka , ikiwemo kugharamia ushiriki wa washindi wa Taifa katika mashindano ya Dunia , japo katika mashindano yote 6 ya Dunia na mengineyo ya kimataifa tume peperusha vyema bendera ya Taifa na Utalii wa Tanzania kwa kutwaa mataji katika mashindano yote tuliyoshiriki, tunashikilia zaidi ya mataji 7 ya Dunia hadi sasa.
Mafanikio haya ya kimataifa matunda yake ni pamoja na Tanzania kupewa heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za Dunia za Miss Tourism World 2006.
Fainali ambazo kwetu zimekuwa kama mwiba wa mchongoma kutokana na watu wengi kudhani kuwa udhamini tulio upata wa serikali ulikuja kwetu, wakati ukweli ni kwamba fedha zili zilikwenda Miss Tourism World Organisation na kulipa watoa huduma wa ndani walio hudumia huduma mbalimbali zikiwemo za malazi, chakula, usafiri, matangazo, ulinzi, kumbi, taa na majukwaa.
Ni kama mwiba wa mchongoma kwetu kwa sababu, wengi wanadhani na kuamini kuwa Miss Utalii Tanzania, tunapata udhamini wa mamlaka za utalii, wakati ukweli ni kwamba hakuna udhamini kama huo.
Licha ya ukweli kuwa katika umri wake wa miaka Miss Utalii Tanzania ndilo shindano lenye mafanikio makubwa zaidi kitaifa na kimataifa kuliko mashindano mengine yoyote nchini na hata Afrika mashariki na kati.
Udhamini ni changamoto na kikwazo kikuu cha kufikia 100% ya malengo ya shindano letu na hata ndoto yetu ya kulifanya kuwa shindano bora zaidi nchini,Afrika na hata Duniani. Baadhi ya mataji ya Dunia tunayo shikilia ni pamoja na Miss Tourism World 20050 - Africa, Tourism Model Of The World 2006- Personality, Miss Tourism World 2006- SADC, Miss
Africa 2006 – 1st Runner Up, Miss Tourism World 2007- Africa, Miss Freedom Of The World 2013, Miss Tourism World 2008 -Internet, Miss United Nation 2009.
Miss Utalii Tanzania ni shindano la kwanza nchini kutwaa taji la Dunia kabla na baada ya uhuru na kuipa Tanzania heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za Dunia 2006.
Rais wa Miss Tourism Tanzania Organisation Gideon Chipungahelo, ni mtanzania wa kwanza kuteuliwa katika uongozi wa ngazi ya Dunia wa Urembo, ikiwemo nyadhifa za Mkurugenzi Bara la Afrika Miss Tourism World Organisation, Miss United Nation Organisation na Makamu wa Rais Dunia World Beauty Pageant Association, Miss Tourism University World Organisation na Miss Heritage World Organisation.
Ili kukabiliana na changamoto hizi, bodi ya mashindano
imebadili sera na mfumo wa uongozi na uendeshaji Mashindano, kutoka katika mfumo wa kuwa shindano la kibiashara hadi kuwa shindano la kijamii (Non Profit Making), kutoka katika mfumo wa kufanya shindano stejini kuanzia ngazi za chini hadi katika mfumo wa kufanya mashindano
stejini kuanzaia katika ngazi za kanda na klanda maalum za vyuo vikuu, kutoka katika mfumo wa kuwa na kamati na mawakala hadi katika mfumo wa kuwa na wakurugenzi waajiliwa wa ngazi za kanda hadi taifa, na kuwa na kamati zenye majina makubwa hadi kamati za wataalam watendaji. Kutoka katika mfumo wa onyesho la viingilio hadi katika mfumo wa onyesho lisilo na viingilio, kutoka katika mfumo wa onyesho la ukumbini hadi katika mfumo wa onyesho la TV Show. Kutoka katika mfumo wa kuweka kambi katika mahoteli hadi katika mfumo wa kuweka kambi katika Miss
Tourism Houses na Tourist Attractions Camp Sites, kutoka katika mfumo wa kuwa shindano la kitaifa hadi katika mfumo wa kuwa shindano la kimataifa, lenye washiriki kutoka mabara yote duniani.
Kwa mfumo huu mpya, washindi wa ngazi za majimbo,wilaya na mikoa watapatikana kwa njia ya Odiashion.
Kwa mfumo huu mpya kila mbunge atakuwa na mrembo wake wa Utalii, Kila Mkuu wa Wilaya atakuwa na Mrembo wake wa Utalii na Kila Mkuu wa Mkoa atakuwa na Mrembo wake wa
Utalii. Lakini pia mfumo huu utadhibiti hujuma na umamluki, udanganyifu wa sifa za washiriki lakini pia kuondoa tatizo la warembo wasio na sifa , wasio na tabia njema na mwenendo mwema katika jamii.
Kwa mfumo huu wa TV Show, fainali zote kuanzia ngazi ya kanda zitarushwa LIVE katika TV na mitandao ya Internet. Aidha kwa mfumo huu tutakuwa na kituo chetu cha Televisheni cha Miss Tourism (Miss UTalii TV).
Mkakati huu, ni mkubwa na unahitaji muda na umakini wa hali ya juu, pia wataalam wa ndani na nje kuufanikisha . Hivyo bodi imeona ni vyema kujipa muda wa mwaka (Msimu) mmoja kujipanga bila ya kufanya mashindano.
Hapa ieleweke kuwa hatuja simamisha shughuli za kampuni za kutangaza na kuhamasisha utalii na utamaduni, bali tumesimamisha shindano la msimu wa 2013/2014, huku washindi wa msimu wa 2012/2013 wakiendelea na majukumu yao kama kawaida , ikiwemo kuwakilisha TaifA katika mashindano ya Dunia na kimataifa 2013/2014 kama ifuatavyo na nchi yanakofanyika katika mabano ni, Miss Tourism World 2013 ( Equatorial Guinea), Miss Face Of The World
2013 ( Afrika Kusini) , Miss Heritage World 2013 (China) Miss Tourism United Nation 2013 ( Marekani), Miss International 2013 ( Japani), Miss Planet 2013 ( Ufaransa ), Miss Tourism University World 2013 (Uingereza).
Aidha bodi imetoa onyo kali kwa yeyote atakaye thubutu au kujaribu tena kuhujumu shiondano hili kwa namna yoyote, kwani atakumbana na hatua kali za kisheria bila ya kujali wadhifa, mamlaka, jinsia au rangi.
Bodi pia imewataka maadui na mamluki wote kujiondoa katika shindano hili na ngazi mbalimbali za uongozi na mataji kabla ya kuondolewa, kwani mchakato ujao hautalengwa kwa jiwe.
Erasto Gideon Chipungahelo
Mwenyekiti Mtendaji
Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO)