HATIMAYE mbivu na mbichi kuhusu utata wa usajili wa mshambuliaji wa yanga, Mrisho Ngassa utajulikana kesho baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kukutana kwa ajili ya kupitia usajili wa wachezaji wa vilabu vinavyoshiriki Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza.
Awali kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa ilikuwa ikutane Agosti 13 na 14 mwaka huu, lakini ilishindikana baada ya kikao cha jana kushindwa kupata akidi.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ina wajumbe saba, na ili kikao kiweze kufanyika ni lazima wapatikane wajumbe kuanzia wanne.
Masikio ya wadau wa soka yatakuiwa na shauku ya kujua hatma ya Ngasa ambaye jina lake limewasilishwa kwa klabu za Simba na Yanga, hivyo kamati hiyo ndiyo itakayotoa jibu sahihi ni timu ipi inastahili kumtumia nyota huyo.
Habari za
uchunguzi zimegundua kuwa klabu ya Simba inastahili
zote za mchezaji huyo kwa kuwa ilikuwa na umiliki wa asilimia 100 wa mchezaji
huyo.
Kwa mujibu wa habari za ndani kutoka kwa mmoja wa viongozi
ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini, alisema Simba ilimchukua Ngasa kwa
mkopo wa asilimia 100 wa sh. milioni 25 ambazo walizilipa Azam na kumchukua
mchezaji.
Mtoa habari wetu alisema baada ya kumchukua Ngasa, Simba
iliingia mkataba wa kisheria ambao unatambulika katika kanuni za mchezaji wa
mkopo na kuwa mchezaji wake halali mara baada ya mkopo kumalizika.