Jumla
ya wanamichezo 58 wamerusha fomu kuomba kuteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule
wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa
upande wa TFF waliorejesha fomu kwa upande wa urais ni Athuman Jumanne
Nyamlani,Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard Rukambura. Nafasi
ya Makamu wa Rais wamejitokeza Imani Omari Madega, Nasib Ramadhan na Walace
Karia.
Walioomba
nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda mbalimbali ni Abdallah Hussein Mussa, Kaliro
Samson, Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona, Vedastus Kalwizira
Lufano, Samwel Nyalla, Epaphra Amana Swai, Mbasha Matutu Mong’ateko, Stanslaus
Haroon Nyongo, Ally Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omari Walii.
Ahmed
Msafiri Mgoyi, Yusuf Hamisi Kitumbo, Ayoub Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius
Kilungeja, Ayoub Shaib Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David Lugenge, Elias
Mwanjala, Eliud Peter Mvela, John Mwachendang’ombe Kiteve, James Patrick
Mhagama, Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William Lugenge.
Athuman
Kambi, Francis Kumba Ndulane, Zafarani Damoder, Charles Komba, Hussein Mwamba,
Stewart Ernest Masima, Farid Salum Nahdi, Geoffrey Nyange, Riziki Majala, Twahil
Twaha Njoki, Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed.
Wengine
ni Alex Chrispine Kamuzelya, Juma Abbas Pinto, Muhsin Balhabou, Omar Isack
Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.
Kwa
upande wa uchaguzi wa TFF mwombaji ambaye hakurudisha fomu ni Venance Mwamoto
pekee.
Kwa
upande wa TPL Board waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni wawili tu; Hamad
Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti).
Walioomba
nafasi za ujumbe wa TPL Board ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael Njunwensi
Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)