MABINGWA wa ligi kuu bara, Yanga Sc leo wamegawana pointi na 'Wagosi wa Kaya' Coastal Union ya Tanga na kujikuta wakitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Aidha, Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc na Wanalamba lamba Azam Fc waliokuwa wakicheza ugenini wamefanikiwa kuondoka na pointi tatu muhimu.
Katika mchezo wa Yanga na Coastal ambao ulitawaliwa na rafu za hapa na pale baina ya wachezaji,timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa 0-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadilikmo ambapo nyota wa kimataifa wa Yanga Didier Kavumbagu, huku timu hizo zikicheza pungufu baada ya wachezaji wake kutolewa kwa kadi nyekundu.
Zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya mwamuzi Martin Sanya kupuliza kipenga cha kumaliza mchezo, Jerry Santo aliisawazishia Coastal kwa penalti.
Nao Simba Sc leo imeondoka na poinbti tatu muhimu baada ya kuwatandika maafande wa JKT Oljoro kwa bao 1-0, a mchezo uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na mfungaji akiwa ni Haruna Chanongo.
Kwa upande wa Azam Fc nao wameweka kibindoni pointi tatu baada ya kuwatandika Rhino ya Tabora mabao 2-0 kattika mchezo ulifanyika uwanja wa Ally hassan Mwinyi na mabao ya Azam yalipachikwa na Gaudance Mwaikimba na Seif Karihe.
Michezo mingine ya ligi hiyo leo ilikuwa ni kama ifuatavyo
MBEYA CITY V RUVU SHOOTING 2-1
MGAMBO SHOOTING v ASHANTI UNITED 1-0
MTIBWA SUGAR V KAGERA SUGAR 1-0
JKT RUVU v TZ PRISONS 3-o