Dar
es Salaam: Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imeleta
msisimko mpya katika utani wa jadi kati ya mashabiki wa Simba na Yanga nchi nzima kupitia kampeni
yake mpya ijulikanayo kama NANI MTANI JEMBE iliyozinduliwa leo jijini Dar es
salaam na itadumu kwa muda wa miezi miwili.
Akiongea kwenye uzinduzi, George Kavishe, Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Premium Lageramesema NANI MTANI JEMBE itawapa fursa ya
aina yake mashabiki wa Simba na Yanga kuonyesha mapenzi yao kwa Simba na Yanga
kupitia kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa sms ambapo Shilingi milioni 100
zitagawanywa kati ya Simba na Yanga halafu fedha hizo zitawekwa katika benki
maalum mtandaoni.
• Kilimanjaro
Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 ambazo zitashindaniwa
Simba na Yanga kupitia mashabiki wake.
• Kampeni
itakapoanza kila klabu itatengewa kiasi cha shilingi milioni 50.
• Katika
kipindi hicho chote mteja ambaye ni Mtani Jembe akibandua ganda la kizibo cha
bia ya Kilimanjaro Premium Lager ataona namba. Ataandika jina la timu yake
(SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo kasha atatuma kwenda
namba 15440 na kuipa shavu timu yake. Baada ya hapo atapata ujumbe wa
kuthibitisha kwamba meseji yake imepokelewa. Kwa kufanya hivyo atakuwa
amepunguza kiasi cha shilingi 1,000 kwenye akaunti ya klabu pinzani na kuiongezea klabu yake kiasi
hicho cha sh. 1,000.
• Mwisho
wa kampeni kama mashabiki wa Simba walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi
Simba itapata milioni 60 na Yanga itapata milioni 40. Na vilevile mwisho wa
kampeni kama mashabiki wa Yanga walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi
Yanga itapata milioni 60 na Simba itapata milioni 40.
• Mteja
anayetuma SMS atachajiwa kiwango cha kawaida cha kutuma sms na baada ya kutuma
sms atapata sms ya uthibitisho kwamba ameipigia kura timu yake na kufanikiwa
kuichangia kiasi cha shilingi 1,000. Kutokana na upigaji kura wa mashabiki,
akiba ya timu wanayoshabikia itakuwa ikiongezeka au kupungua kulingana upigaji
kura.
Mwisho wa kampeni fedha hizo zitakabidhiwa
kwa uongozi wa kila timu kulingana na matokeo ya kura na klabu zitajiamulia
namna ya kutumia fedha hizo.
Kampeni
hii inatarajiwa kuongeza chachu ya ushindani kati ya mashabiki wa Simba na
Yanga kwa kuwapa fursa kuonyesha mapenzi yao kwa timu zao. Mbali na kampeni ya
SMS, kutakuwepo na shilingi milioni 2 ambazo mashabiki watajishindia kila wiki
kwa wiki kumi kwa mashabiki watakaoshiriki zaidi. Vilevile Nani Mtani Jembe itawaburudisha
mashabiki wa Simba na Yanga kupitia matukio mbalimbali mabonanza, promosheni
zitakazofanyika barabarani, kwenye bar na kwenye matawi ya Simba na Yanga. Kampeni
hii itafika kileleni tarehe 14 Disemba 2013 ambapo mechi mechi ya hisani
itachezwa kati ya klabu hizo mbili kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya maelfu ya
mashabiki wa timu hizo.