MEYA WA ILALA AKUTANA NA VIONGOZI WA YANGA


Mstahiki Meya wa Manisapaa ya Ilala Jerry Slaa akisaini kupokea barua kutoka klabu ya Yanga, kulia ni mwenyekiti wa mipango na makazi wa manispaa ya Ilala Sultan Salum
Meya wa Manisapaa ya Ilala jijini Dar es salaam mstahiki Jerry Slaa leo amepokea maombi ya klabu ya Young Africans kuhusu kuomba eneo la ziada kwa ajili ya kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa uwanja wa kisasa eneo la Jangwani.
Mara baada ya kupokea barua hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa bodi ya wadhamani wa klabu ya Yanga Francis Kifukwe, Slaa alisema yeye pamoja na wenzake hawaoni sababu ya kuzuia harakati hizo za maendeleo na faida kwa wanachi wa mkoa wa Dar es salaam.
"Kwanza viongozi wa Yanga poleni sana kwa kuchelewa kufika, nilikuwa nawasubira wenzangu naibu meya pamoja na mwenyekiti wa mipango na makazi wa manispaa ili tuje kuonana na nyie pamoja, kwa kifupi suala lenu litafanyiwa kazi na kufikia mwezi ujao Novemba tayari tutakua tumeshawapatia majibu" alisema Slaa.
Wazee wangu, wanachama pamoja na viongozi suala hili nalikabidhi kwa mwenyekiti wa mipango ili aliwasilishe kwenye kikao cha madiwani na kufikia mwezi ujao tayari majibu yatakua yameshapatikana ili muweze kuendelea na mchakato huo wa maendeleo kwa watanzania.
Akisoma maelezo ya barua mwenyekiti wa bodi ya wadhamini alisema, tumeshangoea na watu wa mazingira na wamemsea wapo tayari kusaidiana na sisi ila kikubwa ni tulikua tunasubiri majibu kutoka manispaa ya Ilala juu ya eneo la ziada tulioliomba.
Mara baada ya kikao hicho cha pamoja katibu wa baraza la wazee mzee Ibrahim Akilimali alitoa shukrani kwa mstahiki meya pamoja wasaidizi wake kwa kuweza kukutana na viongozi wa Yanga na kuweza ahadi ya kulimaliza suala lao la eneo la ziada haraka iwezekavyo.
CHANZO:www.youngafricans.co.tz

Post a Comment

Previous Post Next Post