Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2013
Betty Boniface Omara amekabidhiwa bendera leo na waziri wa mali asili na utalii
mheshimiwa Kagasheki.
Zoezi hili limefanyika katika ukumbi
wa mkutano wa wizara hiyo tayari kwa safari yake ya kwenda kwenye mashindano ya
Miss Universe yatakayofanyika Moscow nchini Urusi mapema mwezi Novemba.
Akimkabidhi bendera huku akimpongeza
waziri Kagasheki pia amemtakia mafanikio mema huko aendako.
Betty pia aliwaahidi watanzania kuwa
mbali na kurudi na ushindi lakini pia ataenda kuitangazia dunia kuacha kutumia
nakshi(Mapambo) yanayotumia pembe za ndovu ili kumaliza tatizo la ujangili
nchini.
Zoezi la kukabidhiwa bendera
lilifanyika likishuhudiwa na Mkurugenzi wa Kitaifa Miss Universe Tanzania Maria
Sarungi Tsehai.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania
2013 yamedhaminiwa na hifadhi ya Taifa Tanapa na Mrembo Betty Boniface
ameshaanza kutangaza hifadhi hizi kwa njia mbalimbali hapa nchini na nje ya
nchi.