Na Dina Ismail
HAKUNA
ubishi kutokuwepo ama kupungua kwa vituo vya kulea vipaji vya michezo nchini
‘Academy’ pamoja na michuano ya mashule kwa ngazi ya msingi (UMITASHUMTA) na
sekondari (UMISSETA) kumechangia kwa kiasi kikubwa kushusha kiwango cha michezo
Tanzania.
Hiyo
inatokana na maeneo hayo kuwa chanzo cha kupatikana kwa wachezaji chipukizi
ambao baadaye wanakuja kuwa tegemeo katika vilabu mbalimbali hapa nchini na
timu za Taifa,kiasi ca kushindwa kufanya vema katika michunao ya kimataifa.
Kutofanya vema
katika michezo pia kumepelekea wadau na
hata makampuni mabalimbali kupunguza nguvu zao katika kutoa sapoti kwa timu ama
timu za Taifa.
Vyama vya
michezo mbalimbali nchini vimekuwa vikilia na makampuni ili kusaidia kudhimini
timu za michezo husika badala ya
kuimarisha upatikanaji wa wachezaji wazuri ambao uwepo wao kwa timu za Taifa
utawavuta kirahisi wadhamini.
Dawa yake ni
kuhakikisha vituo vya kzalisha, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana,pamoja
na michuano ya mashule inarejeshwa kwa kasi na usimamizi wa hali ya juu.
Kwa
kushirikiana na wizara ya habari utamaduni na michezo, vyama hivyo havina budi kuweka
mikakati madhubuti katika taasisi hizo ili baadaye tuanze kupata matunda mazuri
na kurejesha heshima ya Tanzania.
Licha ya
baadhi ya michezo kuonesha kujitutumua katika medani ya kimataifa lakini hali
bado si nzuri sana kwani matunda yake yanatokana zaidi na juhudi binafsi za
mchezaji kwa kusimamiwa na chama chake kwa ukaribu.
Nchi kama
Nigeria, Cameroon, Ghana, Brazil, Misri, Ivory Coast, Marekani, Kenya, Afrika
Kusini na nyinginezo ambazo zinafanya vema kwenye michezo mbalimbali zina vituo
maalum vya kulea vijana pia vyama vyake vya soka na Serikali kuwa na ushirikiano wa karibu katika
kuviendeleza.Na matunda yake tunayaona.
Ikumbukwe katika miaka ya nyuma ambapo
Tanzania ilikuwa ikifanya vema zaidi katika michezo, wengi wa wachezaji
walikuwa wanatokea katika mashindano ya mashule au vituo vya kulea, kukuza na
kuendeleza vipaji.
Baadhi ya
wachezaji nyota walikuwa wakitokea katika vituo hivyo hivyo kuwa rahisi kuwepo
kwa ushindani na ari kwa vijana wanaojifunza ili kuweza kupata namba katika
timu kubwa na hata kuchaguliwa timu za taifa.
Mfano ni
mdau mkubwa wa michezo aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT) Iddi Kipungu alifanikisha kwa kiasi
kikubwa kuzalisha nyota wengi mwishoni mwa miaka ya 1990 ambapo baadhi yao
wanatamba hadi sasa.
Kipingu enzi
hizo akiwa mkuu wa Sekondari ya Makongo alikuwa akisaka wacezaji wenye vipaji
kupitia michauano ya mashule na hata mitaani ambapo aliwachukua wachezaji wenye
vipaji toafauti na kuwaingiza shuleni kwake.
Makongo
ilikuwa kituo bora kabisa cha uzalishaji wa wachezaji mbambali kwa michezo kama
riadha, soka, kikapu, wavi, vishale n.k. Pia
wasanii wa tasnia tofauti ambao kila mmoja alipikwa katika sekta yake na
kuiva vizuri sana, kimichezo na fikra pia.
Uwepo wa
makongo pia ulileta hamasa kubwa ya kuanzishwa kwa vituo mbalimbali vya michezo
ambavyo pia vilijitahidi kwa namna moja ama nyingine kuzalisha nyota
mbalimbali.
Hivyo basi,
baadhi ya timu zilikuwa zikipigana vikumbo kusasijili wachezaji ambao iliwaona
wanafaa kuzichezea timu zao ili ziweze kufanya vema katika michuano
inayoshiriki.
Pia faida ya
Makongo tuliiona hata kwa timu ya Taifa za Taifa za soka na hata riadha kwani
asilimia kubwa ya wachezaji waliokuwemo walitokea hapo.
Taratibu hali ya ubora na viwango vya wachezaji imekuwa ikiondoka na
matokeo yake Tanzania kujikuta inashuka katika medani ya michezo ya kimataifa.
Ni baada ya
Kipingu kustaafu Makongo huku pia vituo vingine vya michezo vikifanya bora
liende kabla ya kupotea kabisa.
Hapo katika
serikali nayo ilipigaga marufuku kuwepo kwa michuano ya mashule hali hiyo nay
ilichangua kushusha kiwang cha michezo kwani mchezaji mzuri huandaliwa tangu
akiwa mdogo.Kwa sasa imerudishwa lakini hali bado si nzuri.
Kwa hali
hiyo ni wakati wa serikali na wadau wa soka kurwejesha hamasa ya michezo kwa
kufufua vituo hivyo, kuanzisha na kusimamia vizuri mashindano ya mashule ili
tuweze kufanya vema na kurejesha heshima ya nchi.
Kwa kuonesha
umakini kutarejesha hata makampuni ama taasisi ambazo zilikuwa zinatoa fedha
kudhamini kabla ya kusitisha kurejea na kutoa sapoti na mwisho wa siku faida
tutaiona.