Na Dina
Ismail
HIVI karibuni
uongozi wa Klabu ya Simba, ulidai
kutokuwa tayari kwa
timu yao kucheza
mechi yoyote na mahasimu wa
jadi Yanga iwapo watatumika waamuzi wa hapa nchini.
Mkuu wa
Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema kwamba
wamefikia uamuzi huo baada ya kuchoshwa na uonevu
wa dhahiri wanaofanyiwa na waamuzi hao kila wanapokutana.
Simba wameliomba
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutumia waamuzi kutoka nje ya nchi katika
mechi zao na Yanga, ili haki itendeke, huku wakitarajia kumuandikia barua
rasmi Rais wa TFF, Jamal Malinzi juu wa
uamuzi wao.
Manara aliweka
wazi kuwa kila wanapocheza na Yanga waamuzi wamekuwa wakiwaonea kwa
makusudi huku wakionesha dhari kwamba
wametumwa.
“Kuna
matukio mengi ya kustaajabisha yamekuwa yakitolewa na waamuzi pindi tunapocheza
na mahasimu wetu, wachezaji wanapewa kadi bila kosa la kueleweka, magoli yetu halali yanakataliwa, wenzetu wanafunga
magoli ya utata yanakubaliwa na mengine mengi”, alisema
Akienda
mbali zaidi, Manara alisema wachezaji wao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vingi
visivyo vya kimichezo na wapinzani wao lakini waamuzi hao wanaishia kuwaadhibu
wachezaji wao tu.
“Tumechoshwa
na hii hali kwa kweli, hatutokuwa tayari kuingiza timu uwanjani iwapo waamuzi
watakuwa ni wale wale”, aliongeza Manara
Manara alisema
watakuwa tayari hata mapato yao yote ya
mchezo wao kutumika kwa ajili ya kugharamia waamuzi kutoka nje kuweza kuchezesha mechi yao ili kuwepo na haki.
Ukiangalia kauli
ya Simba ina mashiko makubwa na hasa ikizingatiwa kuwapo kwa malalamiko ya kuboronga kwa waamuzi si katika mechi za
Simba na Yanga tu hata katika mechi mbaloimbali za Ligi Kuu Kuu Bara.
Mfano hivi
karibuni katika mchezo baina yao katika
duru la kwanza la Ligi Kuu Bara uliopigwa Oktoba Mosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa
sare ya bao 1-1, mwamuzi Martin Saanya alilikataa bao halali la Simba na
kulikubali bao la Yanga ambalo mfungaji aliukumbatia mpira kabla ya kufunga.
Katika mchezo
huo pia Saanya alimtoa nje kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba, Jonas Mkude kwa kadi
nyekundu kabla ya kamati ya Saa 72 ya Uendeshaji na Usimazi wa Ligi kuifuta
baada ya kuona hakufanya kosa.
Kama hiyo
haitoshi, kamati hiyo baada ya kupitia kwa kina ripoti ya mchezo huo, iliamua kumfungia kuchezesha soka kwa miaka miwili Saanya pamoja
na Msaidizi wake, namba moja, Samu Mpenzu ambaye anadaiwa kukataa la Simba lililofungwa na Ibrahim Hajib mapema
kipindi cha kwanza akidai aliotea.
Katika
mchezo huo, maamuzi ya utata ya Saanya yalisababisha vurugu baada ya Yanga
kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe katika
dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya
beki Mbuyu Twite.
Bao la
Tambwe lilizua kizaazaa ndipo wachezaji
wa Simba wakamvaa Saanya wakidai Tambwe
aliushika mpira kabla ya kufunga. Na katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa
kadi nyekundu Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele.
Hali hiyo
ilipelekea mchezo kusimama kwa takriban
dakika tano baada ya mashabiki wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na
kutupa uwanjani kabla ya Polisi kuanza kutumia milipuko ya gesi za kutoa machozi kuwatuliza kabla
ya mchezo kuendelea na Simba kusawazisha
dakika ya 87 kwa bao la Shizza Kichuya.
Kilio kwa
waamuzi haliko kwa Simba peke yao kwani hata Yanga imekuwa ikilalamikia baadhi
ya waamuzi wanaopangwa katika mechi zao na Simba kwa nyakati tofauti huku Simba
ikionekana kuwa muhanga zaidi wa maamuzi tata.
Kwa hali
hiyo, TFF inapaswa kuzingatia na
kulichukulia kwa malalamiko ya Simba ili kuweza kupatikana nusura kwa
soka la Tanzania.