Na Dina
Ismail
HIVI
karibuni kumeibuka tabia inayokera
na kuchefua inayofanywa na
baadhi ya wasanii wa filamu au
wale wa bongo fleva , ikijulikana kama Kiki.
Kitendo
hicho kimekuwa kikitumika zaidi pindi wanapokaribia kutoa nyimbo zao au filamu
zao.
Si jambo baya kwao kutafuta ‘attention’ katika kuelekea kuachia
kazi zao mpya lakini njia wanazozitumia ni
mbaya na sio za kuridhisha.
Msanii kama
kioo cha jamii hana budi kufanya ama kuonesha vitu vizuri ili awe mfano bora
kwa wanaomzunguka lakini si kwa baadhi ya bongo.
Utakuta
msanii anamtukana mwenzake matusi mazito
katika mitandao ya kijamii ama vyombo vya habari au msanii anaweza mzulia
mwenzake jambo lolote la fedheha kiasi cha kuleta picha mbaya katika jamii
lakini mwisho wa siku inakuja bainika kwamba ilikuwa ni Kiki ya kutoa kazi yake
mpya.
Tumeshuhudia
wasanii wakifanya mambo ya aibu sana katika mitandao ya kijamii kinyume na mila
na desturi za Kitanzania na yote hayo wanafanya katika kutafuta umaarufu.
Kweli sasa
hivi sanaa imekuwa ngumu kutokana na hali ya kiuchumi na pia uwepo wasanii
wenye vipaji wanaochipukia kila kukicha kiasi cha kufanya sanaa iwe ngumu.
Na kwa hali
hiyo ndipo wasanii hutafuta njia mbadala za kujiweka matawi ya juu kwa niia
zisizo sahihi ambazo mwisho wa siku inakuwa ni kama dhalili kwao.
Kinachoonekana
hapa ni ufinyu wa fikra na mawazo pia
katika kutayarisha hadi kupakua kazi zao kwani kama msanii yuko vizuri katika
fikra hizo hawezi ‘kutafuta kiki’ ili atoe albamu ama filamu.
Usanii ni
kipaji sasa kama kuna walioingia katika sanaa kwa lengo la kusaka umaarufu au
kuuza sura ndio hao mwisho wa siku wanafanya mambo ya ajabu ajabu.
Mbona kuna
wasanii wengi wanafanya sanaa kwa muda mrefu na majina yao yapo juu na hata
siku moja huwakuti ama kuwaona wakitafuta ‘kiki’ za kijinga wao wanapata
umaarufu kulingana na kazi zao.
Wasanii kama
Mwana Fa, Fid Q, Lady Jaydee, Riyama Ali, Joh Makini, King Majuto ni baadhi ya
wale wanaojielewa kwani hata siku moja huwezi sikia wanatafuta ‘kiki’ wakianza
kutoa kazi zao.
Sana utaona
matangazo ya ujio wao mpya, na pindi kazi ikitoka kama ni nzuri itachukua
nafasi yake kupitia mashabiki na mwisho wa siku heshima yao inabaki kuwa juu.
Pia kuna
wasanii walioibuka miaka ya hivi karibuni kama Darassa, huyu ni mmoja wao
ambaye ubora wa kazi zake umeweza kumuweka katika matawi ya juu ya muziki wa
kizazi kipya.
Kuna njia
nyingi za maana na zenye heshima wanazoweza kupitia katika ‘kuprome’ kazi zao
kama ilivyo kwa wasanii wan chi zilizoendelea badala ya hizi za aibu
wanazozidumia baadhi yao hivi sasa.
Nadhani
ifikie mahala wasanii wanaoishi kwa ‘kiki’ kujipanga upya kuumiza vichwa kwa kutayarisha kazi nzuri na zinazoendana na maadili ya
kitanzania, kinyume na hapo naliona anguko la baadhi yao.
Mungu
Ibariki Tanzania.