TAIFA Stars imeanza vibaya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kutandikwa mabao 3-0 na Morocco katika mchezo wa Kundi F uliopigwa usiku huu Uwanja wa Uwanja wa Laurent Pokou Jijini San-Pedro, Ivory Coast.
Katika mechi hiyo Stars ilimaliza pungufu baada ya kiungo wa Novatus Dismas Miroshi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 70 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Morocco ilijipatia mabao yake kupitia na beki Romain Ghanem Paul Saïss , kiungo Marseille Azzedine Ounahi na mshambuliaji na Youssef En-Nesyri.