Madee, Tundaman kukamua Afrika Kusini




WASANII wa muziki wa kizazi kipya, Madee na Tundaman waliondoka nchini juzi kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya maonyesho mawili ya muziki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, meneja wa Tip Top Connection linalowasimamia wasanii hao, Babu Tale alisema kwamba wasanii hao wamepata mwaliko toka kwa Mtanzania anayeishi nchini humo.

Alisema wakiwa huko wasanii hao ambao hivi sasa wanatamba na singo ya ‘Pesa’ watafanya onyesho lao la kwanza kesho, kabla ya kumalizia jingine keshokutwa.

Madee kwa sasa anatamba na albamu yake ya ‘pesa’ iliyobeba vibao kama ‘mateso zaidi ya yesu’, aliomshirikisha Dully Sykes, ‘mikono juu’, ‘siachi muziki’ aliomshirikisha Makamua, ‘hauridhiki’ aliomshirikisha Z –Anto.

Wakati Tundaman naye akiwa mbioni kuipua albamu yake mpya anatamba na vibao kama ‘Neilah’, ‘nipe ripoti’ , ‘asina’, ‘mapenzi na dhiki’ na nyinginezo.

Post a Comment

Previous Post Next Post