MAKAMU MWENYEKITI WA AZAM, SAID MOHAMMED
UONGOZI wa timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam umesema hauko tayari kumuachia mshambuliaji wao mpya Mrisho Ngassa kurejea katika klabu yake ya zamani, Yanga.
Makamu mwenyekiti wa timu hiyo Said Mohammed alisema kwamba taarifa za baadhi ya wanaowania uongozi katika klabu ya Yanga kuwa wapo katika mipango ya kumerjesha kundini mchezaji huyo hazina ukweli wowote bali ni propaganda za kujipigia kampeni.
Alisema hakuna mjadala wa suala hilo umeshafungwa na hakutakuwa na mazungumzo kuhusiana na mchezaji huyo.
Kwa upande mwingine Azam imetangaza usajili wa wachezaji wake watakaowatumia kwenye msimu mpya na kusema wamesajili wachezaji wapya nane, wamewapandisha toka kuikosi chao cha vijana chini ya miaka 20 wachezaji sita na kuwaacha 10
Wachezaji wapya ni Mohamed Ahmed Binslum, Jackson Chove, Jabir Aziz, Ramadhani Chombo 'Redondo', Kalimangonga Ongala na Ssenyonjo Peter na waliopandishwa daraja ni Tino Augustino, Himid Mao, Mau Alii, Tumba Swed, Ali Mkuba na Samih Alli.