HUSSEIN MACHOZI
TAMASHA kubwa la muziki la kila mwaka FIESTA linatarajiwa kurindima katika mikoa nane ya Morogoro, Arusha, Moshi,Dodoma, Tanga, Dar es Salaam, Zanzibar, na Mwanza.
Ratiba itaanza Julai 7, mkoani Morogoro, kisha Julai 9 litafanyika Matongee Club, Arusha na tarehe 10 litarindima Moshi, Kilimanjaro katika ukumbi wa La Liga.
BAADHI YA WASANII WA TIP TOP CONNECTION
Julai 16 Julai, itakuwa Royal Village, Julai 17 litakuwa uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma , kabla ya Julai 24 kufanyika mkoani Tanga.
Kisha baadaye litahamia jijini Dar es Salaam katika sehemu itakayotangazwa ambapo wasanii wakubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati watashiriki kupamba na kisha litaelekea Zanzibar kwa kufanyika katika bustani ya Forodhani, ndani ya ukumbi wa Ngome na baadaye Musoma
JUMA NATURE
Tamasha litafungwa mkoani Mwanza, Agosti 7 mwezi wa nane, ndani yaukumbi wa Yatch na kumalizika kesho yake katika uwanja wa CCM Kirumba.
Wasanii watakaotumbuiza katika Fistsa 2010 ni pamoja na Diamond,
Belle 9, Hussein Machozi, Baby J, Offside Trick, Chege& Temba, Shaa, Juma
Nature, Dully Sykes, Barnaba, Amini, Linah, Godzilla, Joh Makini, Roma, NikiWa Pili, Young Dee, Fid Q, Mwana Fa, Mataaluma, JCB, Tip Top, Mwasiti, Pina
na Beatrice William.
DULLY SYKES
Fiesta Jipanguse imedhaminiwa na Serengeti Breweries Limited, Precision Air, Prime Time Promotions, Kitangoma Magazine, Mradi wa kuzuia Malaria wa Zinduka, na Clouds FM.