JAJI JOHN MKWAWA, MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI YANGA AKITANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI WA KLABU HIYO
MWENYEKITI wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga, Jaji John Mkwawa amesema kwamba uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika Julai 18, utafanyika katika Ukumbi wa PTA uliopo katioka viwanja vya SAbasaba.
JAJI MKWAWA KULIA na KATIBU MKUU WA YANGA LAWRANCE MWALUSAKO
Alisema kampeni rasmi zitaanza kesho (Julai 7) na wagombea wanatakiwa kuheshimu sheria za nchi kwa kufanya kampeni katika nyakati na vipindi zinasoruhusiwa.
BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI
Jani Mkwawa ameongeza kuwa wagombea LLYOD NCHUNGA, ABEID ABEID, EDGER CHIBULA, MBARAKA IGANGULA, Na FRANSIC KIFUKWE watawania nafasi ya uenyekiti huku AYOUB NYENZI, COSTANTINE MALIGO na DAVIS MOSHA watawania nafasi ya makamu Mwenyekiti.
Wagombea 29 watachuana kuwania nafasi ya ujumbe inayohitaji watu nane.