HISPANIA:MABINGWA WORLD CUP 2010

BAO pekee lililofungwa na Andreas Iniesta katika dakika ya 116, jana liliiwezesha Hispania kutwaa ubingwa wa dunia kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo kwa kuifunga Uholanzi katika mechi ya mwisho ya fainali za Kombe la Dunia zilizoanza Juni 11 na kufikia tamati jana usiku.




Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya wakiutwaa mwaka 2008 kwa kuifunga Ujerumani, ni mara ya kwanza kwa timu iliyofungwa mechi ya kwanza kutwaa ubingwa wa fainali hizi tangu 1930.

Kwa upande wa Uholanzi, ni mara ya tatu kwake kufika fainali bila kutwaa ubingwa kwani ilifanya hivyo mwaka 1974 na 1978.



Hata hivyo, licha ya kufungwa Uholanzi jana ilionyesha soka ya hali ya juu kuanzia mwanzo wa mechi hiyo na kumaliza dakika 90, zikiwa sare ya bila kufungana.

Ushindi huo ni faraja kubwa kwa Kocha wa Hispania, Vicente Del Bosque ambayo ilitua hatua hiyo kwa kuing’oa Ujerumani.



Aidha, ushindi wa Hispania umezidi kumwongezea umaarufu pweza wa nchini Marekani aitwaye Paul kwani Ijumaa iliyopita, alitabiri Hispania kutwaa ubingwa.

Mbali ya Hispani, pweza huyo alitabiri pia timu ya Ujerumani kuifunga Uruguay katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu na ikawa hivyo kwa Uruguay kufungwa 3-2.

Kwa ushindi huo, licha ya Hispania kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza, pia imejitwalia kitita cha dola mil 30 za Marekani,

sawa na shilingi bil 42 za Tanzania.

Wakati Hispania ikiondoka na kitita hicho, Uholanzi imejitwalia dola mil 24 za Marekani, sawa na sh bil 33.6.

SHABIKI WA HISPANIA

Kwa mujibu wa mchanganuo wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia, timu 32 hupata kiasi cha dola mil 1 sawa n ash bil 1.4 za Tanzania.

Mbali ya zawadi kwa timu hizo za juu, pia timu
zilizoishia hatua ya makundi kama ilivyotokea kwa timu za Ivory Coast, Cameroon, Algeria, Afrika Kusini na Nigeria, kila moja imepata dola mil 8 za Marekani, sawa na shilingi bil 11.2 .



Timu zilizoingia hatua ya mtoano, kila moja imepata kitita cha dola mil 9, sawa na shilingi bil 12.6.

Aidha, miamba nane iliyotinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, kila moja iliondoka na kitita cha dola mil 18 sawa na shilingi bil 25.2.

Mchanganuo huo unaonyesha kuwa, timu nne zilizofanikiwa kufika hatua ya nusu fainali, zimepata dola Mil 20, sawa na bil 28 za Tanzania.

HUYU NDIYE SHUJAA WA HISPANIA, INIESTA


Kabla ya kuanza kwa mechi hiyo, burudani kubwa ilikuwa pale Mzee Nelson Mandela, alipowasili kabla ya kuanza kwa mechi hiyo na kuwapungia mashabiki waliokuwa wamejazana kwenye Uwanja wa Soccer City.

Mzee Mandela akiwa na mkewe Graca Machel Nelson Mandela, aliwasili uwanjani na kuusalimu umati uliofurika uwanjani na kulakiwa na vifijo vya vuvuzela huku Mzee Mandela akitabasamu.

1 Comments

  1. poa blog yako ni nzuri na unaenda vizuri, na inapendeza sana kuona akina dada mnachangamka kuanzisha blog zenu, ila nachokushauri dina ni kwamba changanya habari naona ume base kutupa habari za mchezo wa mpira wa miguu, changanya habari mbalimbali za michezo,jamii,burudani, urembo,harusi na matukio ya kusisimua, ukifanya hivyo utawapata wapitiaji wengi katika blog yako,kwa uzoefu wangu wapitiaji wengi wa blogs si washabiki wa mpira machokwambia ndiyo hicho

    ReplyDelete
Previous Post Next Post