MKWASSA
Mkwasa alisema wachezaji 20 kati ya hao ndio watakaokwenda Marekani kwa ajili ya ziara ya kujiandaa na fainali za wanawake zinatakazofanyika Afrika Kusini Oktoba mwaka huu na jumamosi itakwenda Visiwani Zanzibar kuhudhuria tamasha la Sauti la Busara.
Wachezaji hao ni pamoja na Sophia Mwasikili, Fatuma Omar, Mwanaid Tamba, Fatuma Mustafa, Fatuma Bushiri, Mwajuma Abdallah, Asha Rashid ‘Mwalala’, Mwanahamis ‘Omar Gaucho’, Ester Chabruma ‘Lunyamila’, Pulkeria Charaji, Hellen Peter, Frodian Daud, Zena Khamis, Eto Mlenzi, Marry Gabriel, Fatuma Khatibu, Maimuna Said, Fadhila Hamad, Neema Kuga, Evelyn Senkubo, Zahara Kabubure, Mwasiti Juma na Mariam Waziri.
Aliongeza kuwa wachezaji tisa kati ya hao wametoka katika Mashindano ya Shule za Sekondari (UMISETA) ambao ni Mariam Aziz, Donisia Daniel (Dar es Salaam), Semeni Abeid (Tanga), Husna Ayoub (Bukoba), Amina Ali, Mwanaid Saleh Rehema Hussein (Kanda ya Mashariki), Tatu Idd na Shamim Hamis (Kanda ya Kati).