MKUU WA KITENGO CHA TAMASHA NA MAONYESHO, ABRAHAM BAFADHILI
TASWIRA
UKUMBI
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Lewis Makame anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la 29 la Sanaa Bagamoyo linalotarajia kuanza Septemba 27- Oktoba 2 mjini Bagamoyo.
Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Mkuu wa Kitengo cha Tamasha na Maonyesha, Abraham Bafadhili alisema tamasha la mwaka huu linatarajia kushirikisha vikundi 40 vya sanaa mbalimbali vya hapa nchini na nje.