DOGO JANJA ACHEZEA KICHAPO MAKONGO


MSANII kutoka kundi la Tip Top connection Abdulaziz Abubakari ‘ Dogo Janja’ ambaye anasoma Sekondari ya Makongo, juzi alipokea kipigo kitakatifu kutoka kwa mwalimu wake kutokana na kupishana kauli.
Janja anayesoma kidato cha kwanza shuleni hapo alikumbana na kitendo hicho kipindi cha mchana alipokuwa anakwenda kupata chakula cha mchana shuleni hapo.
Chipukizi huyo alikaririwa katika kituo cha redio Clouds na kudai kuwa chanzo cha ugomvi huo ni baada ya mwalimu yule kumuita kwa jina la ‘Dogo Jinga’ na yeye kujibu mapigo kwa kumwambia ‘kubwa jinga njoo’ kitendo ambacho kilimchukiza mwalimu huyo.
Anaongeza kuwa hakuwa akitambua kama yule ni mwakimu katika shule yao kutokana na kutokuwa na muda mrefu tangu ajiunge na shule hiyo, hivyo mwalimu wake kukasirika na kuanza kumtwanga ngumi.
“Nilijua ni mwanafunzi wa vidato vya juu anataka kunizingua, ndiyo maana nikawa namjibu kila alipokuwa ana nitukana na mpaka kuamua kunipiga,” alisema Dogo janja
Dogo alizidi kulalamika kuwa alipigwa sana hasa mdomoni, hali iliyomsababishia maumivu makali mwilini na kwamba alienda hospitali baada ya kushushiwa kipigo hicho.
Ameongeza kusema kuwa ni bora ahame katika shule hiyo kwa ajili ya kukimbia ngumi na mateke aliyoshushiwa na mwalimu huyo, kwani hata baada ya kupelekwa ofisini na mwalimu huyo alianza kumpa maneno ya kejeli mbele ya walimu wote.

1 Comments

  1. Sawa tumemsikia Dogo Janja lakini mwalimu ametumia usemi waarabu wanaoutumia kuwa Altarbiya kabl altaalim yenye maana kuwa ULEZI MAFUNZO YA ADABU KABLA YA KUPEWA ELIMU YA MAENDELEO.mwl katika hekima yake amemfundisha hekima, heshima,adabu na elimu ambayo kijana huyo hataisahau au hata nyumbani kwao hakufundishwa.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post