Kocha mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen alitangaza kikosi cha timu hiyo kinachotarajiwa kuingia kambini kujianda na mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Afrika ya Kati, mechi itakayopigwa machi 26, ambapo mbali na Mgosi baadhi ya wachezajki mahiri walitemwa.
Akizungumza kwa simu kutoka Arusha, Mgosi alisema pamoja na uwezo mdogo, pia anaamini Poulsen bado hajaridhishwa na kiwango chake.
“Mimi naona uwezo wangu ni mdogo kuichezea Stars, ndiyo maana kocha hajaniita, nadhani kiwango chanfgu kipo kwa ajkili ya Simba tu si Taifa Stars hivyo hakuna tatizo lolote mimi kutoitwa katika kikosi cha Stars”, Alisema.