LINEX AWAZIMIA LADY JD, KIDUMU NA RADIO


LINEX
MSANII wa muziki kizazi kipya nchini Sunday Mangu maarufu kama ‘Linex’ amesema iwapo mambo yatakwenda vema anatarajia kuwashirikisha katika albamu yake ya pili wasanii maarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki, Lady Jaydee, Kidumu na Radio kutoka nchini Uganda.
Akizungumza hivi karibuni, mkali huyo alisema tayari ameshaanza matayarisho ya albamu yake hiyo na wakali hao ni miongoni mwa wasanii ambao atawashirikisha katika kazi zake.
“Nawazimia sana wasanii hawa na kama mambo yatakwenda vema nitawashirikisha katika baadhi ya nyimbo zangu zitakazokuwemo katika albamu yangu ya pili, ikishindikana nitafanya hivyo hata wakati mwingine,” alisema Linex.

Post a Comment

Previous Post Next Post