Kituo cha mazoezi cha GENESIS kilichopo kijitonyama jijini DSM kimeandaaa tamasha la mazoezi ya viungo la wazi litakalofanyika tarehe 5 mwezi huu katika viwanja vya LEADRES CLUB jijini DSM.
Mratibu wa tamsha hilo ambaye ni meneja wa kituo hicho SAMUEL KIHAMPA amesema kuwa tamsha hilo hufanyika kila mwaka ,malengo yake yakiwa ni kuwakutanisha wakazi mbali mbali wa jiji la DSM ambao hufanya mazoezi katika vituo mblai mbali vya mazoezi.
KIHAMPA amesema kuwa katika tamasha hilo ambalo litakalo kuwa la bure yaani hakuna kiiingilio, KIHAMPA amesema kuwa tamasaha hilo litafanyika kuanzia saaa moja asubuhi hadi saa nne na nusu.
Watu mbali mbali wameombwa kuja kwa wingi pamoja na familia zao ili kuweza kufanya mazoezi hayo ambayo ni faida kwa afya zao.
Amesema kuwa katika mazoezi hayo zaisdi ya walimu 16 kutoka katika vituo mbali mbali watafundisha kwa muda wa masaaa matatu katika staili tofauti tofauti.
Pia KIHAMPA amesema kuwa katika tamaha hilo kutakuwa na wataalamu wa afya watakaowapima wanamichezo watakaohudhuria tamsha hilo magonjwa mbali mbali yakiwemo kisukari na presha.