ONYESHO LA MAMMA MIA LAIVA, MAMBO YOTE KESHO MOVENPICK


Ijumaa ya tarehe 4 na Jumamosi ya tarehe 5, mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali’ atazindua rasmi toleo lake la kiafrika, katika onyesho kubwa na la aina yake la Mamma MIA, linaloletwa kwenu kwa hisani ya utepe mweupe nchini na ‘Vodacom foundation’.
Onyesho hilo la Mamma MIA lenye lengo la kuchangia na kuhamasisha suala zima la uzazi salama nchini, litafanyika kwa siku mbili mfululizo, toka Ijumaa katika Hoteli ya Movenpick na viwanja vya Mnazi Mmoja kwa siku ya Jumamosi tarehe 5.
Onyesho hilo limepewa jina la ‘Mamma MIA’ kutokana na sherehe za miaka mia moja ya siku ya wanawake duniani, na miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania , kwa madhumuni ya kuhamasisha uzazi salama nchini, na kuzindua rasmi toleo jipya la Mustafa Hassanali.
Akiongea kuhusu maandalizi, Muandaaji wa maonyesho hilo la Mamma MIA, Mustafa Hassanali alisema “tuko katika maandalizi ya mwisho ya onyesho, wageni wetu wabunifu toka nje wameshawasili nchini, na tuko tayari kuwasilisha ubunifu wetu kwa watanzania wapenda ubunifu wa mavazi, na jamii kwa ujumla”
Wabunifu waalikwa ambao wanatarajiwa kuonyesha ubunifu wao siku hiyo, mbali na Mustafa Hassanali, ni Farouque Abdella toka Zanzibar , Minna Hepburn toka Finland na Henrietta Ludgate toka Uingereza, ambapo wao wamezindua mavazi yao katika maonyesho yaliokwisha hivi karibuni ya ‘London Fashion Week’.
“Maonyesho haya tumeyapanga kuanza saa mbili na nusu usiku katika hoteli ya Moevenpick kwa siku ya tarehe nne, na Mnazi Mmoja kuanza saa tisa na nusu kwa siku ya jumamosi tarehe tano mwezi Machi. Aliongezea kusema Hassanali.
Katika kuihusisha jamii katika harakati hizi za kuhamasisha uzazi salama, na kuipa jamii urahisi wa kuona ubunifu huu wa mavazi, mwananchi atakaeshiriki kwa siku ya Jumamosi, atachangia shilingi Mia Moja kama mchango wake, na hii si kwa vinginevyo bali kuchangia utepe mweupe katika harakati za uzazi salama.
Akihamasisha jamii kujitokeza katika onyesho hili la bure na kusisimua la Mnazi Mmoja, Mustafa amesema “hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufanya onyesho kubwa la ubunifu wa mavazi bure, nia yangu ni kuipa jamii hususani wanawake nafasi ya kushiriki katika tukio hili la kihistoria, ambapo siku hiyo onyesho hilo litarushwa moja kwa moja mtandaoni kupitia www.mustafahassanali.net ili na awenzetu waishio nje waweze kushuhudia hili, kwa kweli hii itakuwa ya kwanza katika historia ya bara letu kurushwa hewani kupitia mtandao, na ningependa kuchukua nafasi hii, kuwaomba watu kujitokeza na kushiriki katika tukio hili.”
Vodacom Foundation kama wadhamini, wamekuwa mstari wa mbele katika kuzipa ari jitihada hizi za kusambaza ujumbe wa uzazi salama za utepe mweupe zilizoandaliwa na Mustafa Hassanali
Mkurugenzi Mtendaj iwa wa Vodacom Foundation, Mwamvita Makamba amesema kuwa “Vodacom Foundation mara zote imekuwa mstari wa mbele katika kuisaidia jamii nchini, tunathamini sana juhudi za Mustafa Hassanali katika kuhamasisha uzazi uzazi salama nchini sit tu kwa madhumuni ya kuleta uelewa wa jambo hili, lakini pia kuchangisha pesaa kwa utepe mweupe”
Mamma MIA kwa msaada wa utepe mweupe, ikishirikiana na Vodacom Foundation imedhaminiwa na Johns Hopkins Centre for Communication Programs in Tanzania, The Citizen, Uhuruone, Barclays Bank, Moevenpick Royal Palm Hotel, C2C,Ultimate Security, Novamedia, Darling Hair, Vayle Springs, Eventlites, Fashion 4 Health, image masters and 361 Degrees.

Post a Comment

Previous Post Next Post