MISS TANZANIA 2010 GENEVIEVE EMMANUEL AENDA KUSAIDIA YATIMA KAGERA




Mrembo wa Taifa Vodacom Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel anaondoka leo asubihi na ndege kwenda Mkoani Kagera, kwa kazi za jamii.

Akiwa mkoani Kagera mrembo huyo wa taifa ataungana na warembo wengine wa Mkoa wa Kagera kutoa misaada katika vituo vya kulelea watoto yatima cha Umri Yatima na Nusura Yatima vilivyopo Bukoka mkoani Kagera.

Miss Tanzania 2011 Genevieve Emmanuel atakabidhi misaada ya vyakula, pamoja na vifaa vya kusomea kama vile vitabu, madaftari, chaki, kalamu n.k.
Hadi hivi sasa mrembo huyu wa Taifa ameshatoa misaada ya kibinadamu katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma, na D'salaam.
Kabla hajamaliza muda wake kwa mwaka huu, amepanga kutembelea mikoa ya kusini Lindi na Mtwara.

BEAUTY WITH PURPOSE ndiyo kaulimbiu ya mashindano ya urembo ya Tanzania na Dunia kwa ujumla.


HIDAN .O. RICCO,

Ofisa Habari
0715 / 0755 019288

Post a Comment

Previous Post Next Post