WEMA SEPETU ATIWA MBARONI KWA UTOVU WA NIDHAMU





Aliyekuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu (27) , mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la kutukana hadharani.


Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alimtukana matusi ya nguoni msanii wa kizazi kipya, Raheem Rummy 'Rais wa masharobaro' ambapo mshitakikosa lake.


Hata hivyo mshitakiwa huyo alidai mahakamani hapo kuwa aliamua kumtukana mshitakiwa kwa sababu ya dharau zake alizokuwa anamfanyia.


''Mheshimiwa Hakimu si kawaida yangu kutukana ovyo ovyo, lakini hasira zimenifanya nifanye hivyo na ndiyo maana nimekubali kosa langu.


Mbele ya Hakimu Mariamu Masamalo, ilidaiwa na Karani Sharifa Dunia kuwa, Aprili 11 mwaka huu Kinondoni, mshitakiwa alimtukana mlalamikaji huyo na kesi imehairishwa mpaka Aprili 18 mwaka huu.
Wema Sepetu katika pozi.



Mshitakiwa huyo anafikishwa mahakamani hapo kwa pili, ambapo awali alimfanyia fujo msanii wa filamu, Steven Kanumba baada ya kuvunja kioo cha gari.Miss huyo aliachiwa kwa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili kwa sh. 300,000 kila mmoja.

1 Comments

  1. Hii ni mpya hivi kutukana hadharani ni kosa Tanzania. Ipo kwenye kifungu gani cha sheria?

    ReplyDelete
Previous Post Next Post