ASAMOH APELEKA KILIO MSIMBAZI, AIPA YANGA UBINGWA WA KAGAME 2011

BAO pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Kenneth Asamoah katika dakika ya 108 leo liliipa Yanga taji la nne timu hiyo katika michuano ya klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati ‘Kagame Castle Cup 2011’ baada ya kuwalaza wapinzani wao wa jadi Simba kwenye Uwanja wa taifa, jijini Dar es Salaam. 
Asamoh aliifunga bao hilo muda mfupi baada ya kuingia katika mechi hiyo akimpokea Jerry Tegete,  alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha krosi ya Rashid Gumbo iliyojaa upande wa kulia wa mlindamlango mahiti mchini Juma Kaseja.

Aidha, furaha zaidi ilikuwa kwa kocha Mganda anayeinoa Yanga Sam Timbe ambaye amezidi kujiwekea rekodi ya pekee katika michuano hiyo kwake ikiwa taji la nne anashinda na klabu nne tofauti

Timbe aliyejiunga na Yanga katikati ya msimu uliopita na kuiwezesha kutwaa ubingwa bara,  alianza kuipa ubingwa Kagame Sc Villa ya Uganda mwaka 2005 Mwanza, baadaye Polisi ya Uganda mwaka 2006,jijini Dar es Salaam na mwaka 2009 mjini Khartoum, Sudan aliipa Atraco ya Rwanda.

Yanga jana ilistahili yshindi kwa sabnabu ilicheza kwa utulivu na umakini wa hali ya juu lakini tatizo lililosababisha kuwacheleweshea ushindi ni umaliziaji mbovu wa washambuaji wake Davies Mwape, Tegete, na Hamis Kiiza ambao walipoteza nafasi za dhahiri zosiozopungua tatu.

Yanga ambao walichukua tena ubingwa miaka ya  1975, 1993 na 1996 kwa ushindi huo wamezawadiwa dola za kimarekani 30,000 pamoja na kombe huku Simba ikipata dola 20,000 na El Merreikh iliyonyakua dola 10.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwa dakika 120 baada ya ikiwa ni baada ya kumalizika dakika 90 kwa suluhu ya bila kufungana, mwamuzi Wiish Yabarow  wa Somalia alimzawadia kadi ya njano Amir Maftah kwa utovu wa nidhamu.

Aidha, Simba nayo itajilaumu kwa kuishindwa kutumia vena fasi ilizozipata kupiotia kwa Musa Mgosi, Mwinyi Kazimoto ambaye aliumukia katika mchezo huo na kukimbizwa hospitali baada ya kukanyagana na Juma Seif, hali iliyopelekea jahazi la Simba kupotea na hasa nafasi ya kiungo.

Aidha, pamoja na vituko vya hapa na pale kutokea katika mechi hiyo, mpigapicha mkuu wa gazeti hili Joseph Senga alipata mshikemshike kutokana na kuvaa nguo za njano na hivyo kutakiwa aondoke katika langi la Simba alipokuwa amekaa akiendelea na kazi yake,huku wakati zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi likiendelea umeme ulikatika na hivyo kulazimika watumie mwanga toka katika gari la wagonjwa lililokuwepo uwanjani hapo.


Simba: Juma Kaseja, Nasoro Said, Amir Maftah,  Kelvin Yondani,  Juma  Nyoso, Patrick Mafisango,  Shija Mkina, Mwinyi Kazimoto,  Haruna Moshi, Mussa Hassan Mgosi na Ulimboka Mwakingwe

Yanga: Yaw Berko,  Shadrack Nsajigwa, Godfrey  Taita Oscar Joshua, Chacha Marwa, Nadir Haroub, Nurdin Bakari, Jerry Tegete, Davies Mwape, Juma Seif/Rashid Gumbo na Hamis Kiiza .

Aidha, katika michuano hiyo timu ya El Merreikh ya Sudan ilitwaa nafasi ya tatu baada ya kuifunga mabao 2-0 St.George ya Ethiopia katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ambapo mabao ya El Merreikh yalifungwa Jonas Sakwaha na Saeed Mustafa katika dakika ya 48 na 54.

 Timu nyingine zilizoshiriki michuano hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) na Rais Paul Kagame ni Vital O (Burundi), Etincellers (Rwanda), Ocean View (Zanzibar), Red Sea (Eritrea), Bunamwaya (Uganda), Elman F.C (Somalia), APR (Rwanda), Ulinzi (Kenya) na  Ports (Djibout).

Post a Comment

Previous Post Next Post