BOBAN, MWAIKIMBA WACHUNGULIA TAIFA STARS

WAKATI kikosi cha timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ kitakachoivaa Algeria kikitarajiwa kutajwa Julai 31, kocha mkuu wa timu hiyo Jan Poulsen amekusudia kuwaita kundini washambuliaji Haruna Moshi ‘Boban’ na Gaudance Mwaikimba.

Poulsen aliwaambia waandishi wa habari leo kwamba Boban (Simba), Mwaikimba (Moro United) pamoja na Juma Seif Kijiko wa Yanga, amewongeza katika kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana wenye Umri chini ya Miaka 23 ili kuangalia uwezo wao kama unakidhi kuwemo Taifa Stars.

“Wachezaji hawa nimekuwa nikiambiwa uwezo wao,  kabla ya kuwaita nahitaji kuona viwango vyao hivyo wataungabna na timu ya vijana katika maandalizi ya mechi yake na Shelisheli na mimi nitakwenda Arusha na nitataja kikosi baada ya mechi hizo,”Alisema.

Poulsen aliongeza kuwa iwapo ataridhishwa na kiwango cha wachezaji wataorodheshwa katika kikosi kipya kitakachoingia kambini Agosti 2 kujiandaa na mechi yake ya kirafiki dhidi ya Palestina itakayopigwa Agosti 10 katika jiji la Ramallah.

Post a Comment

Previous Post Next Post