mshambuliaji wa Tanzania Mrisho Ngassa (kushoto) wa Seattle Sounders FC ya Marekani, akichuana na mlinzi wa Manchester United Fabio Da Silva
LICHA ya kujitahidi kufurukuta jana kwa kwa mshambuliaji wa Tanzania, Mrisho Ngassa,ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani akijifua na klabu ya Seattle Sounders Vancouver White Caps, hakuweza kufua dafu kwa Manchester United.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Century Link, Sounders ililala kwa mabao 7-0, Ngassa aliingia dakika za lala salama ambapo Wayne Rooney, alifunga mabao matatu ‘hat-trick’ ndani ya dakika 21 za mwisho wakati Michael Owen, Mame Biram Diouf, Gabriel Obertan na Park Ji-sung kila mmoja alitundika bao moja.
United ipo nchini Marekani kwa ziara ya kimichezo ambapo ilianza kwa kucheza Los Angeles Galaxy na kuitandika kwa mabao 4-1, huku kesho inatarajiwa kusafiri hadi Chicago na baadaye itaenda New Jersey kabla ya kuhitimisha ziara yao kwa kucheza katika jiji la Washington.