FM ACADEMIA KATIKA USIKU WA HALUA NA TENDE VATICAN CITY KESHO

BENDI ya muziki wa dansi nchini ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ kesho inatarajiwa kutoa burudani katika onyesho lilikobatizwa kama ‘Usiku wa Halua na Tende’, litakalorindima kwenye ukumbi wa Vatican City, uliopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Afrika Kabisa Entertainment (AKE) iliyoandaa onyesho hilo, Robert Ekerege, alisema jana kuwa onyesho hilo ni mahususi kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki wa huko sambamba na kutambulisha nyimbo zao mpya.
Alisema nyimbo hizo zipo katika albamu yao mpya iitwayo ‘Chuki ya Nini’ ambapo ndani yake kuna vibao kama Fataki, Ndoa ya Kisasa, Dai chako ulaumiwe na Chuki ya nini uliobeba jina la albamu.
“Si onyesho la kukosa kwa wadau wa muziki na hasa ule wa dansi kwani kama mjuavyo mambo ya FM Academia si ya utani, njooni mpate burudani ya kutakata,” alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post