JULIO ATANGAZA JESHI LA KUIVAA SHELISHELI


KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 Jamhuri Kihwelo Julio (wa kwanza kushoto) akitaja kikosi cha timu yake kitakachoivaa Shelisheli julai 27 na 30 katika dimba la Sheikh Amri Abeid,Arusha.
Kikosi hicho kitaingia kambini kesho kabala ya kuondoka Julai 25 mwaka huu kwenda Arusha tayari kwa mechi zake hizo zi kirafiki.
Kihwelo amewataja wachezaji hao kuwa ni pamoja na Shabani Kado (Yanga), Seif Abdul (African Lyon), Juma Seif (Mtibwa Sugar), Babu Ally (Morani), Shomari Kapombe (Polisi Morogoro), Issa Rashid (Mtibwa Sugar),Salum Kanoni (Simba), Godfrey Wambura (Simba), Jabir Aziz (Azam) na Awadh Juma (Mtibwa Sugar).

Wengine ni Mohamed Soud (Toto
Africans), Salum Machaku (Simba), Salum Mnyate (Azam), Khamis Mcha (Azam),Thomas Ulimwengu, Sino Augustino (African Lyon) na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).

Katika hatua nyingine, timu ya Taifa ya  Shelisheli inatarajia kuwasili Arusha kesho mchana ikitokea Nairobi, Kenya ikiwa na  msafara wa watu 30 wakiwemo wachezaji 24 na viongozi sita.

Wachezaji ni hao ni pamoja na Nelson Sopha, Vincent Euphrasie, Jonathan Bibi, Nigel Freminot, Allen Larue,
Ronny Marengo, Gervais Waye Hive, Achille Henriette Karl Hall,Alex Nibourette, Jude Nancy, Jones Joubert, Alpha Balde, Nelson Laurence, Trevor Poiret, Henny Dufrene, Don Anacoura, Kevin Betsy, Brian Dorby,
Wilnes Brutus, Eugene Valentin, Rashim Padayachy, denis Barbe na Damien Maria

Post a Comment

Previous Post Next Post