Kocha Moses Bases |
KOCHA mkuu wa Simba Moses Basena ametamba timu yake kutwaa ubinwa wa Kagame katika mechi ya fainali baina yao na mahasimu wao wa Jadi, Yanga utakaopigwa kesho kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Basena amesema anajivunia ubora ilichonacho kikosi chake ambacho kimekuwa kikiimarika na kuwa tishio kila kukicha katika michuano hiyo.
"Kila kitu kumekaa sawa wachezaji wangu wana ari kubwa na mechi hiyo na kutokana na maandalizi mazuri niliyowapa sambamba na kufanyia marekebisho kasoro za hapa na pale, ushindi ni lazima", Alisema.