SAFARI ya mshambuliaji wa kimtaifa wa Simba Mganda Emmanuel Okwi kusajiliwa na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kuenda ikaota mbawa.
Hiyo anatokana na mshambuliaji huyo kushindwa kufanyiwa vipimo vya afya kama inavyoelekezwa sheria za usajilui wa wachezaji pindi wanapojiunga na timu kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa.
Habari zilizopatikana toka ndani ya uongozi wa Simba zinasema kwamba, licha ya Okwi kufaulu majaribio ya uwanjani lakini suala la kitofanya vipimo vya afya kuenda ikafuta nafasi hiyo.
Mmoja ya viongozi wa Simba amesema kwamba Okwi hakupata kufanyiwa vipimo vya afya kutokana na sababu zisizoelezeka ambapo kumekuwepo na taarifa tofauti juu ya hatua hiyo.
Okwi kwa sasa yupo kwao Uganga alipokwenda baada ya kufiwa na anatarajiwa kuja nchini mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuanza kujinoa na Simba huku akiendelea kusubiria mustajkabali wake ndani ya Kaizer Chiefs.