REDD'S MISS TEMEKE KULAMBA MIL.2


 MKURUGENZI WA BMP PROMOTIONS BENNY KISAKA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO, KULIA NI MENEJA WA BIA YA REDD'S VICTORIA KIMARO
 WASHIRIKI WA MISS TEMEKE KATIKA POZI

MREMBO atakayetwaa taji Miss Temeke mwaka 2011 ataondoka na fedha taslim shilingi mil.2.Shindano linatarajiwa kufanyika jumamosi kwenye ukumbi wa TCC Chang'ombe.

Mkurugenzi wa BMP Promotions inayoandaa shindano hilo, Benny Kisaka amesema kwamba wameamua kutoa zawadi ambazo zitakidhi mahitaji ya warembo hao kulingana na hali ilivyo sasa.

Alisema, mshindi wa pili atapata shilingi mil.1.5, huku mshindi wa tatu atapata shilingi mil.1, wakati mshindi wa nne na wa tano kila mmoja ataondoka na shilingi 500, 000, huku walisalia kila mmoja atapata kifuta jasho cha shilingi 200,000.

Alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo litakaloshirikisha warembo 15 toka vitongoji vya Chang’ombe na Kurasini yamekamilika ambapo mwaka huu pia taji la Miss Tanzania litatua Kanda ya Temeke.

“Tumejiandaa vema na hasa katika suala la warembo kwa kweli wana sifa zinazostahili kutwaa taji la Miss Tanzania kurithi mikoba ya Geneviev Mpangala”, Alisema Kisaka.

Taji la Miss Temeke linashikiliwa na Geneviev ambaye pia anashikilia taji la Miss Tanzania 2010/2011, huku Cynthia Kimasha, Elizabeth Boniface, Eunice Mbuya, Husna Twalib, Irene Jackson, Joyce Maweda, Lucia John, Mwajuma Juma, Naifat Ally, Naomi Ngonya, Prisca Stephen,  Sasha Seti, Sara Said, Sara Paul na Victoria Mtega watawania taji la Miss Temeke.

Aidha, Kisaka alisema shindano hilo ambalo limedhaminina na Kampuni ya bia Tanzania kupitia bia ya Redd’s, Vodacom, Gazeti la Jambo Leo na Sally Saloon, litapambawa na burudani toka kwa B-Band na msdanii wa Bongo Fleva, AT.

Post a Comment

Previous Post Next Post