REDD'S MISS TEMEKE WATAKIWA KUTOCHAFUA HALI YA HEWA

 BAADHI YA WASHIRIKI WA MISS TEMEKE KATIKA POZI
 KUTOKA KUSHOTO NI MENEJA WA REDD'S VICTORIA KIMARO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA ZIARA YA WAREMBO WA MISS TEMEKE WALIPOTEMBEA OFISI ZA TBL AMBAO NI WADHAMINI WA KUU WA SHINDANO HILO KUPITIA KINYWAJI CHA REDD'S , KATIKA KATI NI MENEJA MASOKO WA TBL FIMBO BUTALLAH NA KULIA NI MKURUGENZI WA BMP PROMOTIONS INAYOANDAA MISS TEMEKE, BENNY KISAKA
                                              
WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la kumsaka Redd’s Miss Temeke 2011 wametakiwa kuwa na tabia njema pindi wanapomaliza shindano hilo ili kutochafua hali ya hewa katika jamii.
Hayo yalisemwa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah jana, wakati warembo hao walipotembelea kambuni hiyo inayodhamini shindano hilo kwa ajili ya kujifunza.
Alisema, wakiwa kama mabalozi wa kinywaji cha Redd’s, wanatakiwa kuonyesha tabia nzuri katika jamii, badala ya kutafuta umaarufu kwa kufanya vitendo viovu, ambavyo vinaharibu tasnia hiyo.
“Hatutegemii baada ya hapa mkachafue majina yenu, kwani mabalozi wetu hawana sifa mbaya katika jamii, mnalo jukumu la kukitangaza kinywaji hiki kwa kufanya mambo yaliyo na heshima katika jamii,” alisema Butallah.
Aidha, wakiwa kiwandani hapo, walipata nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali, ikiwemo jinsi ya uzalishaji wa bidhaa za kiwanda hicho, ikiwemo kinywaji cha Redd’s.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Jumamosi katika ukumbi wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam, ambako warembo 14 watachuana kuwania taji linaloshikliliwa na Genevive Mpangala, ambaye pia anashikilia taji la Miss Tanzania.
Warembo watakaowania taji hilo ni pamoja na Cynthia Kimasha, Elizabeth Boniface, Eunice Mbuya, Husna Twalib, Irene Jackson, Joyce Maweda, Lucia John, Mwajuma Juma, Naifat Ally, Naomi Ngonya, Prisca Stephen,  Sasha Seti, Sara Said, Sara Paul na Victoria Mtega.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa BMP Promotions inayoandaa shindano hilo, Benny Kisaka alisema, maandalizi yanakwenda vema na kwamba, mpaka sasa mbali na TBL ambao ni wadhamini wakuu kujitokeza, wengine ni Vodacom Tanzania ambao pia ni wadhamini wakuu wa Miss Tanzania, gazeti la Jambo Leo na  saluni ya kisasa ya Sally iliyopo katikati ya Jiji.

Post a Comment

Previous Post Next Post