TWIGA STARS, BANYANABANYANA NA ZIMBABWE KUNDI MOJA ALL AFRICAN GAMES


SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limepanga makundi ya michuano ya All African Games, ambapo timu ya taifa ya Tanzania ya wanawake ‘Twiga Stars’ imepangwa kundi B.
Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 3 hadi 18 mwaka huu jijini Maputo nchini Msumbiji, ambako Twiga imepambanishwa na Afrika Kusini ‘Banyana Banyana’, Ghana na Zimbabwe, wakati kundi A kutakuwa na wenyeji Msumbiji, Cameroon, Guinea pamoja na Algeria.
Kwa upande wa wanaume, kundi A litakuwa na wenyeji Msumbiji, Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’, Libya na Madagascar, wakati B kutakuwa na Cameroon, Uganda, Ghana na Senegal.
Twiga Stars ambayo ilifuzu fainali hizo baada ya wapinzani wao Kenya, Uganda na Sudan kujitoa. Katika kujiweka sawa kwa mashindano hayo, Twiga hivi karibuni ilishiriki michuano ya COSAFA huko Zimbabwe, ambako ilikutana na wenyeji na kufungwa kwa changamoto ya penalti 4-2 na Banyana Banyana bao 1-0 hatua ya nusu fainali.

Post a Comment

Previous Post Next Post