Mratibu wa mashindano ya riadha yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2011’, Zaituni Ituja (kushoto) wa Kampuni ya Capitalplus International (CPI) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui na katikati ni Mkurugenzi wa Maliasili wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ibrahim Musa aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri wake Ezekiel Maige.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui (kushoto) akipokea baadhi ya vipeperushi kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Maife Kapinga wakiwa kama miongoni mwa wadhamini kwa ajili ya mashindano ya ‘Rock City Marathon 2011’ wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano hayo uliyofanyika Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui (kulia) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika uzinduzi wa mashindano ya Rock City Marathon 2011 uliofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maliasili wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ibrahim Musa aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri wake Ezekiel Maige.