MWAPE AWACHINJA SIMBA

BAO pekee la mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Davies Mobby Mwape katika dakika ya 72, jana lilizima ngebe za wapinzani wao wa jadi, Simba SC baada ya kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo mbali na Yanga kulipa kisasi cha kufungwa 2-0 na mahasimu wao hao katika mechi ya Ngaio ya Jamii, Agosti 17, mwaka huu, lakini umewafanya wapunguze tofauti ya idadi ya pointi wanazozidiwa na watani wao hao katika msimamo wa ligi. Baada ya kila timu kucheza mechi 12, Simba inaendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi zake 27, wakati Yanga ina pointi 24 sasa. Yanga; Yaw Berko, Oscar Joshua, Chacha Marwa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Seif ‘Kijiko’, Nurdin Bakari, Haruna Niyonzima, Davies Mwape/Jerry Tegete, Kenneth Asamoah/Rashid Gumbo na Hamisi Kiiza/Idrisa Rashid.  Simba: Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’/Patrick Mafisango, Juma Jabu, Juma Nyosso, Victor Costa, Jerry Santo, Shomary Kapombe, Amri Kiemba/Haruna Moshi ‘Boban’, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi na Ulimboka Mwakingwe/Ulimboka Mwakingwe.

13 Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHOctober 29, 2011 at 10:25 PM

    POLENI SANA WANYAMA KUMBE KWELI MANJI NDIO KIBOKO YENU,PAMOJA NA KUUNDA KAMATI ZENU ZA HARUSI ZA KINA ZITTO KABWE NA WENGINE LAKINI MMESHINDWA NA MTU MMOJA TU TENE MHINDI..POLENI SANA,HILO NDIO SOKA,SASA MJIANDAE KUTUPISHA HAPO JUU

    ReplyDelete
  2. HAHAHAHA POLE DADA NAJUWA UMEANDIKA BASI NA ROHO INAKUUMA MAANDISHI UMEANDIKA KIDOGO..ILA ANGEKUWA SIMBA UNGEANDIKA MPK CHINI TUPENI HABARI KAMILI SISI TULIO MBALI NA HUKO BONGO..DAH...YANGAA OYEE HATA HIVYO ACHA KUBANA

    ReplyDelete
  3. NASIKIA JANA WANYAMA MMEPIGANA TENA...KUMBE SIKU HIZI TUTAKUA HATUWAFUNGI,KAMA KILA TUKIWAFUNGA MNAPIGANA HAINA HAJA YA KUWAFUNGA,BORA MUIMARISHE ILE TIMU YENU YA MASUMBWI PALE CLUB,SIMBA BOXING CLUB

    NDONDI:HARUNA MOSHI VS EMANUEL OKWI

    MAFISANGO VS ............

    ADEN RAGE VS NYANGE KABURU

    ReplyDelete
  4. WAVUTA BANGI HARUNA MOSHI NA MAFISANGO NASIKIA WAMEMTANDIKA OKWI.....SIMBA BWANA,HUYO HARUNA SIMBA INABIDI WAFANYE MAAMUZI MAGUMU KAMA WALIYOFANYA YANGA KWA CHUJI!!!!HANA ADABU KABISA YULE KIJANA,ALIPELEKWA ULAYA BADALA YA KUCHEZA MPIRA AKAWA ANAWATEMEA MATE WAZUNGU!BANGI YA KUVUTIA CHOONI MBAYA SANA,IMEMUHARIBU KABISA YULE KIJANA

    ReplyDelete
  5. WADAU WA YANGA WOTE TUKUTANE NYUMBANI KWETU LOUNGE MACHOZI BAND JUMAMOSI IJAYO...KUTAKUA NA BONGE MOJA LA PARTY KAMA KAWAIDA YETU BILA KUPIGANA MATEKE NA NGUMI TUTASHEREHEKEA KISTAARAB KUWAPAKATA TENA HAWA JAMAA,SISI TUNAWAPIGA MAENEO MUHIMU SIO KWENYE NGAO NA VYETI VYA KWENDA KUWAONYESHA WABUNGE...TUKUTANE PALE MAHALI PETU PA RAHA JUMAMOSI IJAYO..KAMA KAWAIDA NGUO ZA NJANO NA KIJANI KWA KWENDA MBELE

    ReplyDelete
  6. ZILE KAMATI WALIZOUNDA SIMBA WIKI ILIYOPITA ZILIKUA NI KAMATI ZA MAZISHI HAYA YA JANA AU?

    ReplyDelete
  7. haruna kama kweli amefanya ushenzi huo afukuzwe

    ReplyDelete
  8. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHOctober 30, 2011 at 4:17 PM

    TATIZO LA WANYAMA UBAHIRI,WE BADALA YA KUIPELEKA TIMU KWENYE KAMBI MAENEO YANAYOELEWEKA WAO WAKAIPELEKA UBUNGO WAKATI WENZAO YANGA MANJI ALIWAPELEKA MASAKI!!!!NILISEMA MIMI JUZI HILO TU TAYARI LILIKUA GOLI LA KWANZA,MASAKI NA UBUNGO WAPI NA WAPI,HATA HIVYO POLENI SANA ILA HAPANA KUPIGANA MKIFUNGWA!

    MDAU WA BOMBA USA

    ReplyDelete
  9. Fatuma Mtanga-u.s.a.October 30, 2011 at 4:20 PM

    kumbe hata simba inafungwaga....!!!du mi nilikua sijui..basi poleni mwaya!

    ReplyDelete
  10. pole sana mama simba dina zuberi ndio mpira ulivyo!

    ReplyDelete
  11. Mpaka aibu...aibu aibu, sijui ulitokaje uwanjani, pole sana.

    ReplyDelete
  12. tatizo unaipenda simba kupita kiasi,hiyo timu itakuua kwa presha mdogo wetu...hamia azam kama mimi dadako

    ReplyDelete
  13. mwee hurumaaa mpe pole asha kigundula na somoe,wamama mnaipenda simba vibaya nyie sina hamu,lakini ndio yamewakuta tena mashostito poleni mwaya,karibuni nyumbani kwetu yanga lounge,machozi band jmosi ijayo tutakapokua tunaselebuka kushangiliwa kuwapakata tena,complementary zenu mtazikuta mlangoni.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post