SIMBA WAJIBU MAPIGO YA MANJI

SIMBA kupitia kamati zake mpya mbalimbali imejibu mapigo ya mfadhili wa Yanga, Yusuf Manji ambaye ameapa kuhakikisha heshima ya klabu hiyo hiyo inarejea chini ya ufadhili wake kwa klabu hiyo ambapo moja ni kuhakikisha wanashinda mechi zake za ligi kuu ya vodacom zilizobaki.
Jana wajumbe wa kamati hizo zinazoundwa na vibosile mbalimbali wakiwemo wabunge,wafanyabiashara na wadau maarufu wa timu hiyo wamekubaliana kwa kauli moja kuipa sapoti ya kutosha timu yao ili iweze kushinda michezo yake yote minne iliyobaki kwenye ligi hiyo.
"Tumedhamiria kushinda mechi zote zilizobaki na katika mechi hiyo ile ya Yanga nayo ipo ndani yake,"Alisema mmoja ya wajumbe wapya wa kamati za Simba.

7 Comments

  1. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHOctober 18, 2011 at 8:08 PM

    MI NAONA "MJUMBE MMOJA" MUOGA...KWANINI ASIJITOKEZE HADHARANI KAMA YUSUF ALIVYOFANYA KWA YANGA AMBAPO ALITOKEZA HADHARANI NA PICHA YAKE UKAIWEKA HAPA...HAO AKINA "MJUMBE MMOJA" WANAOGOPA NINI?WANAMUOGOPA MTU MMOJA YUSUF MANJI PEKE YAKE AU?

    SAYZ MDAU WA YANGA BOMBA,GRAND RAPIDS,MICHIGAN CITY,USA.

    ReplyDelete
  2. Dada wewe Simba mbaya wewe, yaani unashibikia vibaya wakati ukijua kabisa soccer letu la bongo ni siasa tu...sasa wana siasa na mpira wapi na wapi? wewe zito tangu lini au Makala akawa mtu wa mpira...tutabaki tunapiga kelele hivi hivi, mashindano ya kimataifa tunatolewa raundi ya kwanza...tunapata bahati ya rufaa nako tunatolewa tunaanza siasa mara hili mara lile...hatuwezi kupiga hatua yeyote ile.

    ReplyDelete
  3. Hayo ndio mambo mazuri tunayoyahitaji katika michezo hapa Tanzania. kwa hali hiyo tutaendelea kimichezo.

    "TUACHE MAJUNGU NA CHUKI KATIKA MICHEZO"

    ReplyDelete
  4. "mmoja wa wajumbe wapya" nae anatuzingua tu...na kwa nini kamati mpya ziunde baada ya manji kurejea yanga?hivi kweli tunamuogopa manji kiasi hiki wanasimba mpaka kufikia kumuundia kamati?shame on us!!!!!!tunampa ujiko wa bure tu hana lolote yule..

    ReplyDelete
  5. mimi mnyama damu lakini sikubaliana na hii idea ya kutumia nguvu nyingi kwenye taifa starz wakati simba pia inahitaji hiyo nguvu...hili ndio tatizo la kuwa na viongozi wa vilabu wanasiasa..hapo lengo na mtu anatizama interest zake za kisiasa kutaka kuitumia national team kupata cheap popurarity kwa mustakabali wake wa kisiasa siku za usoni,ya simba yametushinda tutayaweza ya national team kweli,mi nasema hivi kama tunahisi tunazo nguvu za kutosha wanasimba tuzielekeze simba,taifa starz iko well organized tayari,ina sponsors wa uhakika na kila kitu,simba hapa safari za kwenda nje tu mpaka leo lazima tupitishe bakuli kwenye maofisi ya watu, leo eti tunataka kuifadhili national team!!!sio kweli.

    ReplyDelete
  6. Naungana na mdau wa kwanza hapo juu. Kwa kweli huu upenzi wetu wa simba na yanga sijui tu ni kwaajili ya soccer la ndani...sababu tukitoka nje ya Africa tumefika sana raundi ya pili. Sasa dada yangu Dina na yeye anashabikia idea za kijinga za Rage, huyu yupo kisiasa tu, sasa anatudanganya kuwa wana mpango wa kujenga ghorafa 12...vipi uwanja...alisema tunajenga uwanja wa kisasa...jamani hatutaki siasa, mbona Azam wanafanya taratibu bila maneno....sisi aha, ghorafa, Rage kaunda kamati, aha, Zito ndani ya Simba...Zito ni nani bwana....tunataka maendeleo na siyo maneno tu.

    ReplyDelete
  7. watu wa simba kwa vishindo utawaweza?

    ReplyDelete
Previous Post Next Post